Home Kitaifa KAGERA YAUNGANA NA WANAWAKE WENGINE DUNIANI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA WANAWAKE

KAGERA YAUNGANA NA WANAWAKE WENGINE DUNIANI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA WANAWAKE

Theophilida Felician, Kagera

Ikiwa leo Tarehe 8 Machi mwaka 2024 wanawake Duniani kote wakisherehekea sikukuu ya wanawake, wanawake wa Mkoani Kagera ni miongoni mwa wanawake hapa nchini walioshiriki sherehe hizo kwa ukamilifu.

Sherehe hizo zilizofanyika viwanja vya Kaitaba Manispaa ya Bukoba, kimkoa zimewakutanisha wanawake mbalimbali kutoka nyanja tofauti tofauti wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Fatma Mwassa.

Katika maadhimisho hayo zimetolea hotuba kadha wa kadha ikiwemo ya Mkuu wa Mkoa ambaye awali amewapongeza akina mama wote waliojitokeza nakushiriki sherehe hiyo.

Amesema kuwa Tanzania inayoongozwa na Rais mwanamke Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya mengi ya ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo hapa nchini na Kagera ambapo ameitaja baadhi yake kwa upande wa Kagera ikiwemo ya Barabara, Shule mpya za Msingi/ Sekondari, Hospitali 8 za Halmashauri zote 8 miradi ya maji ukiwemo mradi mkubwa wa Rwakajunju unaojengwa Halmashauri ya wilaya Karagwe na mingine mingi.

Hata hivyo ametoa wito akiwasihi wanawake Mkoani humo kuendelea kusimama imara katika suala zima la uwajibikaji.

Awali Mbunge mstaafu wa jimbo la Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka akitoa hotuba yake amewasisitiza wanawake kuendelea kuwa shupavu, kujiamini, kujisimamia katika mambo yote bila ya kuteteleka kwani wanawake ni nguzo muhimu katika jamii.

“Mwanamke siyo kulialia unalialia wewe ni Mto Kagera?” amehoji Prof. Tibaijuka huku washiriki wakimshangilia kwa makofi.

“Wanawake wenzangu hampaswi kulialia hovyo mimi kufikia hapa nimefanya kazi nyingi na kubwa katika nchi hii na huko nje ya nchi yote hii ni bidii nakujiamini hivyo tuyazingatie haya kwa dhati” ameendelea kutoa mengi Prof. Tibaijuka

Katika hotuba yake hakusita kutoa ujumbe wakukemea suala la fitina na maneno maneno ya uongo katika ujenzi wa maendeleo Kagera kwani ni mambo ambayo siyo mazuri na hayafai kabisa.

Hotuba nyingine nikutoka kwa Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Bukoba Mhe Emakulata Banzi yeye licha ya mengi pia amekemea changamoto ya adha ya Rushwa ya ngono kwa kundi la wanawake kwani ni miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakiwakabili wanawake hivyo yapaswa kuyakemea kwa nguvu zote huku akiwataka kutokukubali jambo hilo kwani mafanikio ya mtu ni juhudi zake mwenyewe.

Maadhimisho hayo yamepambwa na nyimbo zenye jumbe za kuchochea maendeleo ya mwanamke na kuchezwa na wanawake viwanjani humo na Mkuu wa Mkoa. Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake ni “Wekeza kwa mwanamke kuharakisha maendeleo”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!