Home Kitaifa KAFULILA AFUNGA KIKAOKAZI CHA WATAALAMU WA PPP

KAFULILA AFUNGA KIKAOKAZI CHA WATAALAMU WA PPP

Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. David Kafulila, akizungumza wakati akifunga rasmi kikaokazi kati ya Serikali na Wataalam kutoka Taasisi ya Benki ya Dunia inayojihusisha na utoaji wa mikopo na misaada ya kiufundi kwa Sekta Binafsi – International Finance Corporation (IFC), kilicholenga kupitia na kujadili miradi ya kimkakati ambayo Serikali inataka itekelezwe kwa njia ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kilichofanyika kwa siku 5 katika Ukumbi wa  Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi wa Uwekezaji na Huduma za Ushauri wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kutoka Taasisi ya Benki ya Dunia inayojihusisha na utoaji wa mikopo na misaada ya kiufundi kwa Sekta Binafsi – International Finance Corporation (IFC) Bi. Ramatou Magagi, akifundisha namna ya kuandaa miradi ya PPP, manunuzi Pamoja na namna ya kuandaa mikataba bora ya miradi ya ubia, kwa wataalam wa kitanzania kutoka TANESCO, TPA, DART, TRC, TANROADS, Wizara ya Madini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Vyuo vikuu vya Mzumbe na UDSM, TGDC na TPDC wakati wa kikaokazi kinachoendelea katika Ofisi Ndogo za Hazina Jijini Dar es Salaam, kikihusisha Serikali na Wataalam hao kutoka IFC.
Afisa Mwandamizi wa Uwekezaji Sekta ya Kimataifa ya Nishati kutoka Taasisi ya Benki ya Dunia inayojihusisha na utoaji wa mikopo na misaada ya kiufundi kwa Sekta Binafsi – International Finance Corporation (IFC) Bw. Stefan Rajaonarivo, akifundisha namna bora ya kuandaa miradi ya nishati kupitia njia ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kwa wataalam wa kitanzania kutoka TANESCO, TPA, DART, TRC, TANROADS, Wizara ya Madini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Vyuo vikuu vya Mzumbe na UDSM, TGDC na TPDC wakati wa kikaokazi kinachoendelea katika Ofisi Ndogo za Hazina Jijini Dar es Salaam, kikihusisha Serikali na Wataalam hao kutoka IFC.
Mtaalam wa masuala ya Ubia kutoka Taasisi ya Benki ya Dunia inayojihusisha na utoaji mikopo na misaada ya kiufundi kwa Sekta Binafsi – International Finance Corporation (IFC) Bi. Caroline Eric, akifundisha namna ya kuandaa miradi bora na yenye sifa ya kuvutia mitaji kutoka sekta binafsi (PPP) kwa wataalam wa kitanzania kutoka TANESCO, TPA, DART, TRC, TANROADS, Wizara ya Madini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Vyuo vikuu vya Mzumbe na UDSM, TGDC na TPDC wakati wa kikaokazi kinachoendelea katika Ofisi Ndogo za Hazina Jijini Dar es Salaam, kikihusisha Serikali na Wataalam kutoka IFC.
Wadau mbalimbali wa masuala ya Ubia kutoka taasisi mbalimbali za Serikali wakimsikiliza kwa umakini Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. David Kafulila akifunga rasmi kikaokazi kilichofanyika kwa siku 5 kati ya wataalam hao wa Serikali na Wataalam kutoka Taasisi ya Benki ya Dunia inayojihusisha na utoaji wa mikopo na misaada ya kiufundi kwa Sekta Binafsi – International Finance Corporation (IFC), katika Ofisi Ndogo za Hazina Jijini Dar es Salaam, kikihusisha Serikali na Wataalam hao kutoka IFC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!