Home Kitaifa JUMUIYA YA WAZAZI MARA YAFIKISHA ELIMU YA MAADILI KWA WANAFUNZI

JUMUIYA YA WAZAZI MARA YAFIKISHA ELIMU YA MAADILI KWA WANAFUNZI

Na Shomari Binda-Musoma

JUMUIYA ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi( CCM) mkoa wa Mara imefanya ziara ya kutembelea shule za msingi na sekondari kutoa elimu ya maadili kwa wanafunzi.

Ziara hiyo imefanyika kuwlekea maadhimisho ya wiki ya wazazi ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo mei 5.

Akizungumza kwenye shule ya sekondari Morembe, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa wa Mara,Julius Magubo,amesema maadili yameshuka hivyo hakuna budi kufikisha ujumbe.

Amesema vitendo vya ushoga na usagaji vimekuwa vikitokea kwa jamii huku walengwa wakiwa vijana na wanafunzi kubakwa jambo ambalo linatakiwa kukemewa.

Magubo ambaye alikuwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo,amesema jukumu la kutoa elimu ya maadili lifanywe na kila mmoja kuanzia wazazi na walezi majumbani.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa jumuiya hiyo taifa, Mgore Miraji,amewataka wanafunzi hao kusema hapana na kutoa taarifa pale watakapofuatwa na mtu kuhusiana na kujihusisha na vitendo vya ushoga na usagaji.

Amesema vitendo vya ushoga na usagaji ni kinyume cha maadili na hakikubariki kwa jamii na kuwataka wanafunzi kujihepusha navyo.

Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira manispaa ya Musoma ambaye pia ni diwani wa viti maalumu Asha Muhamed amesema mmomonyoko wa maadili uliopo kwa sasa umetokana na wazazi na walezi kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Amesema wazazi na walezi wanapokuwa kwenye majukumu yao ya utafutaji wa riziki wakumbuke malezi ya watoto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!