Na Neema Kandoro, Mwanza
Jumuiya ya Maendeleo Kilimanjaro (JUMAKI) wamekutana katika Uwanja wa ccm kirumba chini ya kiongozi wao mkuu ambaye ni mangi mkuu Deogratias Ngowi kujadili ajenda ya maendeleo yao.
Kikao kilichofanyika Leo Jijini Mwanza ambapo walijadili maendeleo mbalimbali walioyafanya katika jumuiya hiyo na kubadili baadhi ya masuala yaliyokuwa hayana tija kwa jumuiya hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mangi Mkuu, Deogratias Ngowi Alipata fursa ya kuelezea mambo mbalimbali walioyafanya katika jumuiya hiyo,ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari Jumaki secondary school, Jumaki insurance na Bima ya mkopo ambapo uwekezaji huo umefanyika maeneo ya Buhongwa.
Hata hivyo kiongizi huo amewataka wanajumuiya wote kufika katika maeneo hayo kujipatia hutuma ili waweze kuunga mkono miradi hiyo,Pia kiongizi hiyo alitumia nafasi hiyo kuwaalika wakazi wa Mwanza kujiunga na shule yao kwa mwaka wa masomo 2024 kwa kidato cha kwanza kwani shule ni nzuri ikiwa na walimu wabobezi na mazingira ya kujifunza ni mazuri.
Mangi mkuu huyo alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wachaga wote waishio Mwanza kujiunga na jumuiya hiyo ya jumaki kwani ni yao haibagui na pia alimshukru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali yake kwa ushirikiano wanaotoa kwa jumuiya hiyo.
Mwenyekiti aliwashukru wanajumuiya wote waliohudhuria katika kikao hicho kwani walionesha moyo wa kuwatia moyo viongozi kuwa wanaupenda umoja wao.