Home Kitaifa JUMLA YA MIRADI 2,099 YASAJILIWA NA TIC ILIYOZALISHA AJIRA 539,488.

JUMLA YA MIRADI 2,099 YASAJILIWA NA TIC ILIYOZALISHA AJIRA 539,488.

Na Deborah Lemmubi.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bwana Gerson Msigwa amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi februari 2025 Tanzania kumekuwa na idadi kubwa usajili ya miradi katika sekta zote ambapo jumla ya Miradi ya uwekezaji 2,099 imesajiliwa katika kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na jumla ya Ajira 539,488 zimezalishwa na Mitaji iliyowekezwa ndani ya nchi ina thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 25.098.(sawa na takribani Shilingi Trilioni 67).

Msigwa amesema hayo leo Machi 16,2025 katika Mkutano wake na Wanahabari uliofanyika Bandari kavu ya Kwala Mkoani Pwani wakati akielezea masuala mbalimbali yaliyotekelezwa na Serikali.

Ambapo ameongeza kuwa miradi mipya 1,982 imeanzishwa miradi ya ubia imefikia 476 Miradi upanuzi wa uwekezaji ni 117,huku miradi ya Watanzania ikiwa 719 na Miradi ya wageni ikiwa 904.

Naomba nitoe takwimu chache za kuthibitisha ongezeko kubwa la uwekezaji nchini mwetu. Katika kipindi cha kuanzia Machi, 2021 hadi Februari, 2025 Tanzania imeshuhudia idadi kubwa ya usajili wa miradi mbalimbali katika sekta zote kama ifuatavyo;- Jumla ya miradi ya uwekezaji 2,099 imesajiliwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Jumla ya ajira 539,488 zimezalishwa, Mitaji iliyowekezwa ndani ya nchi ina thamani ya Dola za Marekani Bilioni 25.098 (Sawa na takribani shilingi Trilioni 67)”.

Jumla ya miradi mipya 1,982 imeanzishwa,Miradi ya ubia imefikia 476Miradi ya iliyohusisha upanuzi wa maeneo ya uwekezaji ni 117Miradi ya Watanzania ni 719Miradi ya wageni ni 904“.

Aidha amegusia Sekta ya viwanda ambayo ndiyo sekta inayoongoza kwa uwekezaji nchini kwamba kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi kufikia Februari, 2025 jumla ya miradi ya viwanda 951 imesajiliwa ambapo Miradi hii inatarajiwa kuleta ajira 124,339 na kuwekeza mitaji ya Dola za Marekani Bilioni 10.5 (Sawa na takribani shilingi Trilioni 27).

Pia ameeleza kuwa Mkoa wa Pwani unashika nafasi ya pili katika kuvutia uwekezaji hapa Nchini ukitanguliwa na Mkoa wa Dar es Salaam ambapo katika kipindi cha miaka minne Mkoa huo umepokea Miradi ya Uwekezaji 369 wakati asilimia 67 ikiwa ni miradi ya Viwanda ambayo jumla yake imefikia 247 ambapo Mitaji iliyowekezwa katika sekta zote kwa Mkoa huo ni Dola za Kimarekani Bilioni 4.6.

Ndugu Wanahabari; Mkoa wa Pwani unashika nafasi ya pili katika kuvutia uwekezaji nchini ukitanguliwa na mkoa wa Dar es Salaam. Katika kipindi cha takribani miaka minne kuanzia mwaka 2021 hadi Feb 2025 Mkoa wa Pwani, umepokea miradi ya uwekezaji 369 ambapo kati ya hiyo asilimia 67 ni miradi ya viwanda ambayo jumla yake imefikia 247″.

Aidha, mitaji iliyowekezwa na sekta zote kwa mkoa wa Pwani ni dola za Marekani Bilioni 4.6 (sawa na shilingi Trilioni 12.4) ambapo asilimia 61 ya mitaji hiyo inatokana na sekta ya viwanda ikiwa na mitaji ya dola za Marekani Bilioni 2.8 (sawa takribani shilingi Trilioni 7.5)”.

Huu ni moja kati Mikutano ya Msemaji Mkuu wa Serikali ambayo amekuwa akiifanya na Waandishi wa Habari kuelezea mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali na hasa Serikali ya awamu ya sita chini Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!