Home Kitaifa JUKWAA LA WAZALENDO HURU LAWAKUMBUKA WANAWAKE WAFUNGWA LINDI

JUKWAA LA WAZALENDO HURU LAWAKUMBUKA WANAWAKE WAFUNGWA LINDI

Na Scolastica Msewa, Kibaha.
Jukwaa la Wazalendo huru mkoa wa Pwani Waadhimisha siku ya Mwanamke duniani kwa kwenda kupeleka msaada wa mahitaji mbalimbali muhimu katika gereza la wanawake la mkoa wa Lindi kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhudumia wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kibaha kabla ya kuanza safari ya kwenda kupeleka msaada huo Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wazalendo Huru Tanzania Khadija Juma amesema katika kuhakikisha uzalendo unasambaa nchini hufanya matukio mbalimbali yatakayoonyesha uzalendo katika taifa la Tanzania.

Kwa kuigusa jamii kwa namna tofauti ikiwa ni pamoja na kusaidia watoto yatima, wazee, waliopo magerezani, waathirika wa dawa za kulevya na kuhamasisha uzalendo zaidi kwa lengo la kuhakikisha watanzania wote tunakuwa wazalendo na kuendelea kuunga mkono serikali yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anayoyafanya ili taifa liwe salama.

“Tunahakikisha tunaigusa jamii kwa namna tofauti ili twende pamoja ili taifa letu linakuwa salama hivyo katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani tunatoa msaada wa mahitaji muhimu kwa wafungwa wakike waliopo katika gereza la mkoa wa Lindi” Hadija alisema.

Kundi la wafungwa wanawake ni miongoni mwa makundi yaliyosahaulika katika jamii hivyo wao waliaamua kuandaa misaada ya vitu mbalimbali ili kuwapelekea wafungwa wakike walipo katika gereza hilo ilikuonyesha upendo kwao katika siku hiyo muhimu kwa wanawake duniani”.

Amesema taasisi hiyo ilianzishwa kwa lengo la enzi waasisi wa taifa hili kuunga mkono kazi nzuri zinazofanywa na viongozi wa taifa letu la Tanzania katika awamu zote sita.

Aidha amewaomba Wanawake kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia katika masuala mbalimbali anayofanya yakuendeleza taifa letu.
Mwenyekiti wa jukwaa la wazalendo huru mkoa wa Pwani Ivan Rutatina alisema jukwaa hilo katika mwezi huu wa kuonyesha upendo kwa kudi la Wanawake wameandaa matukio mbalkimbali ikiwemo ziara ya kwenda kupeleka msaada huo kwa wafungwa wanawake wa mkoa wa Lindi.

Alisema waliona wasaidie serikali kwa kupeleka msaada huo kwa wafungwa wa kike ambao mara nyingi huwa wanasahaulika sisi tukiwa ni Jukwaa la wazalendo huru tumeona tupeleke msaada huo gerezani.

Katibu wa Jumuhiya ya Wananwake wa jukwaa hilo la Wazalendo Huru Hawa Mcheka alisema kusaidia wenye mahitaji nchini ni moja ya malengo ya jukwaa hilo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!