Home Kitaifa JUKWAA LA THE WARRIOR WOMEN   LAWAFUNDA WAJASIRIAMALI ZANZIBAR

JUKWAA LA THE WARRIOR WOMEN   LAWAFUNDA WAJASIRIAMALI ZANZIBAR

WANAWAKE Visiwani Zanzibar wameshauriwa kujiamini na kujikubali katika kuanzisha biashara za Ujasiriamali wakitumia ubunifu wa rasilimali zilizopo kisiwani humo kutengeneza bidhaa ambazo wataziuza ndani na  nje ya nchi bila kufanana katika biashara moja.

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mgeni Hassan Juma, ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Wajasiriamali lililoandaliwa na taasisi ya The Warrior Women ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya wanawake ambayo kidunia hufanyika Machi” 8.

Amesema Zanzibar imebarikiwa kuwa na vitu vingi vya asili vinavyoonesha utamaduni wake ambavyo kimataifa vinatumika lakini bado wanawake hawajawa na uthubutu wa kuanzisha biashara.

“Kabla hujafanya biashara kwanza jiamini, usiogope kupata changamoto anzisha biashara zako kwa ubunifu wako tuache biashara za kugana maana hujui mwenzio anaifanyaje biashara hiyo,” amesema

Amesema kuna mabadiliko makubwa katika serikali kuweka sera ambazo zitaweza kuwasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi hivyo watumie fursa hiyo kujifunza mbinu tofauti kutoka kwa wengine waliofanikiwa ili wainuke kuchumi.

 “Elimu haina mwisho na elimu sio kusoma skuli tu bali ni kujifunza mambo mbalimbali ambayo yatawasaidia kuwa wafanyabiashara wazuri na wazalishaji wazuri wa bidhaa zenu.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwanzilishi wa Taasisi ya The Warrior Women, Sabra Issa Machano, amesema taasisi hiyo imejikita kuwainua wajasiriamali kimasoko na kuwasaidia kupeleka bidhaa zao dunia nzima ili wakue kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Amesema wazo la kuandaa jukwaa hilo la pili ni kwa ajili ya kuwaweka pamoja wajasiriamali kusaidiana kwenye fursa kujifunza na kuungana na wadau mbalimbali ili kusogeza mbele harakati zao za kijamii.

Mkurugenzi wa Taasisi ya The Warrior Women Sabra Issa Machano akizungumza na Wanahabari katika Ukumbi wa Bolilo Visiwani Zanzibar mara baada ya kuzindua rasmi msimu wa pili wa jukwaa la Wajasiriamali

Naye Mrajis wa Asasi za Kiraia, Ahmed Khalid, amesema serikali inathamini jitihada zinazofanywa na wajasiriamali ambapo tayari wameanza kutambuliwa kwa kupewa vitambulisho maalumu na kupewa mikopo.

Amesema ni vyema wajasiriamali wanapopata majukwaa hayo kutumia fursa zilizopo katika mkusanyiko huo ambao wataweza kuboresha shughuli zao wanazozifanya za ujasiriamali.

Nao baadhi ya wajasiriamali akiwemo Halima Mhando Rajabu anayeuza vipodozi amesema licha ya kuwepo changamoto za mitaji na masoko, wajasiriamali wanatakiwa wasikate tamaa na kujifunza mbinu tofauti ili kuweza kufika mbali zaidi.

…..Mwisho..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!