Home Kitaifa JOYCE MANG’O ATAKA WABUNGE KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

JOYCE MANG’O ATAKA WABUNGE KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

Na Shomari Binda-Musoma

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kupitia kundi la wanawake, Joyce Mang’o, amewataka wabunge na viongozi wengine kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa mjini Musoma mara baada ya kukabidhi zaidi ya shilingi milioni 4 kwa vikundi 4 vya ujasiliamali vya Kata ya Kitaji.

Amesema huu ni wakati wa wabunge na viongozi wengine kuwasaidia wanawake waweze kuinuka kiuchumi kwenye maeneo mbalimbali na sio kuwasubili kama ngazi wakati wa uchaguzi.

Mang’o amesema wanawake wakiwezeshwa kwenye shughuli zao za ujasiliamali wanazozifanya wanayo nafasi ya kuinuka kiuchumi na kusaidia familia.

Amesema vikundi ambavyo vimewezeshwa Kata ya Kitaji ana imani vitafika mbali na kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa tayari vilishaanza kujishughulisha na ujasilimali na kiasi cha fedha walizopata kitasaidia kuongeza mtaji.

Niwakumbushe wabunge na viongozi wengine kutumia nafasi zao kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuwa ni ngozo kubwa kwenye familia”

Nikupongeze sana Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kitaji,na diwani wa Vito maalumu,Asha Muhamed, mmeandaa jambo kubwa katika kuviinua vikundi vya Kata yenu na uwe mfano wa kuigwa kwa vikundi vingine mkoani Mara”, amesema Mang’o.

Aidha mjumbe huyo wa NEC amepokea wanawake 12 kutoka vyama vya upinzani na kujiunga na CCM na kudai iwapo vikundi vya wanawake vikiwemo vya UWT vikiwezeshwa vitawavutia wanawake wengi kujiunga na chama hicho.

Akikabidhi mitungi 30 ya gesi kwa wanawake wa Kata ya Kitaji,Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Mgore Miraji,wanawake wakiinuliwa kiuchumi wanaweza kufanya mambo makubwa.

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Mara, Nancy Msafiri, amewapongeza viongozi hao kwa kuwa mstari wa mbele kuwainua wanawake na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,katika kuwainua wanawake.

Diwani wa viti maalumu kanda ya Mukendo, Asha Muhamed, amesema wakati wakiandaa shughuli hiyo na Mwenyekiti wa Kata ya Kitaji UWT hawakutegemea kama jambo hilo litakuwa kubwa kama ilivyotokea.

Kwa upande wa vikundi 4 ambavyo viliwezeshwa kuongezewa mitaji wameshukuru viongozi hao na kusema kiasi cha fedha walichopewa kinakwenda kuwaunganisha zaidi kwenye shughuli zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!