Home Kitaifa JOKATE ACHANGIA SHILINGI MILIONI 7 MBINGA

JOKATE ACHANGIA SHILINGI MILIONI 7 MBINGA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Jokate Mwegelo amechangia kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya muendelezo wa ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbinga.

Vilevile, Jokate amechangia kiasi cha shilingi milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT wilaya ya Mbinga.

Katibu Mkuu Jokate amechangia michango hiyo alipokuwa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma kwenye ziara yake ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo.

Aidha, amehimiza kuendelea kuwa na umoja katika kufanikisha ukamilishwaji wa ujenzi wa ofisi na nyumba hiyo kwani uwepo wa ofisi utasaidia katika kufanya kazi kwa ufanisi katika ushirikiano wa ukaribu pamoja na utunzaji wa nyaraka katika hali ya usalama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!