Na Magrethy Katengu
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imewashauri wananchi wote kupenda bidhaa zinazozalishwa Tanzania kwani zimeboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya juu zaidi kwa kutengenezwa na huuzwa ndani na nje ya nchi .
Ushauri huo umetolewa Jijini Dar es salaam katika Sikukuu ya Sabasaba na Mwalimu anayetoa mafunzo ya utengenezaji bidhaa za ngozi kutoka chuo cha Dakawa kilichopo Morogoro Hamidu Nahembe wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao ambapo amesema Sasa Tanzania iko vizuri kiteknolojia kutumia malighafi zake kutengeneza bidhaa zinazouzwa ndani na nje ya nchi na ni bora zaidi .
“Tunatengeneza bidhaa mbalimbali kupitia ngozi ya Mbuzi, Ng’ombe ikiwemo Mabegi ya ofisini,Mikoba ya akina mama, Viatu, vifaa vya kuwekea funguo, mikanda ya kiunoni, na teknolojia tunayoitumia ni ya juu hivyo tunajitahidi kutoa mafunzo kwa vijana wetu na wamekuwa wakiajiria na kuajiriwa Viwandani ikiwemo Kiwanda cha Bora hivyo wazazi watambue kuwa Veta ni sehemu nzuri ya kuwapatia watoto wao ujuzi” amesema Mwalimu Hamidu
Naye Mwalimu wa Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Chuo cha Dakawa Morogoro Theodora Kiungu amesema Wakulima kupitia Ufugaji kwa kutumia teknolojia ya uzalishaji ufugaji itawasaidia kujikwamua kiuchumi hivyo ni vyema kujinga kozi fupi katika chuo wapatiwe mafunzo ya kutumia teknolojia ya kisasa kuanzia kufunga Nyuki hadi utengenezaji bidhaa zake
“Nyuki Wanafaida kubwa sana ila wananchi wamekuwa wakifunga Nyuki kizamani sana na hawajui kuwa kila zao la nyuki ni fedha wakati mwingine hata Asali yao kutokana kutofahamu namna ya kuichuja vizuri na kuihifadhi hushindwa kukidhi Kimataifa hivyo nawasisitiza kuongeza ujuzi hakuangalii umri jiungeni mpate mafunzo ili mjikomboe kiuchumi” amesema Theodora
Aidha Ufugaji wa nyuki una faida kubwa na hutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo nta, mafuta, mishumaa hivyo kitokana na ari ya Serikali ya awamu ya Sita imefungua milango ya uwekezaji na biashara sasaTanzania ni nchi Mungu ameibariki kuwa na Malighafi nyingi za uzalishaji bidhaa mbalimbali hivyo Veta ipo kwa ajili ya kusaidia kutoa mafunzo ya uzalishaji bidhaa zinazokidhi kiwango cha kimataifa.