Na Magrethy Katengu
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikiongeza jitihada za makusudi kwa kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kutoa Elimu Ili kuhakikisha ifikapo 2030 vifo vitokanavyo na Ugonjwa wa kifua viwe visiwepo kabisa.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Dkt. Reginald Mlay wakati akifungua Mafunzo ya Wanahabari kuelekea Maadhimisho ya Kifua kikuu Machi 24 mwaka huu juu ya Ugonjwa wa kifua kikuu amesema jitihada zote inayofanya serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya njema hivyo inatambua kuwa baadhi ya magonjwa siyo wote wangeweza kutibiwa ikiwemo TB, Ukimwi hivyo imekuwa ikitoa fedha kuchangia mfuko wa pamoja ndiyo maana magonjwa hayo huduma hutolewa bure.
“Hakuja jambo lisilokuwa na changamoto hivyo pamoja na jitihada za Serikali ikishirikiana na wadau lakini bado tatizo lipo hivyo tutahakikisha tunashirikiana na Waandishi wa habari kusambaza Elimu juu ya Ugonjwa huu ambao umekuwa ukisababisha tunapoteza nguvu kazi ya Taifa unakwisha kabisa kwani tumejipanga sisi na idara ya Afya “amesema Dkt. Mlay
Kwa upande wake Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Jiji la Dar es salaam Dkt Mbarouk Seif amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 yenye wagonjwa wengi wanaougua ugonjwa wa Kifua kikuu kwa mujibu wa Takwimu wagonjwa laki Moja thelathini na saba elfu hugundulika kwa mwaka huku vifo thelathini na mbili hutokea kwa mwaka na themanini na saba kwa siku Moja na 33 ni watu waliokuwa na maambikizi ya TB na HV.
Dkt Seif amesema tatizo la kifua kikuu limekuwa likiathiri uchumi wa nchi kwa kuligharimu 7% ya pato la Taifa hivyo lazima kuwe na ushirikiano wa pamoja kutokomeza janga hilo kwani ugonjwa huu huambukiza kwa njia ya hewa endapo mgojwa hajaanza matibabu dalili zake ni ikiwemo kutoka jasho jingi,Kukohoa makohozi yenye damu,kupunguza uzito,homa za usiku hivyo mtu yeyote anapoona dalili Moja kati ya hizo awahi kupima kituo cha Afya.
“Mgonjwa ambaye hajapata matibabu ana uwezo wa kuambukiza watu kati ya 10-20 hivyo ni vyema endapo kati ya Jamii anayoishi nayo wakigundua miongoni mwao ndugu,jamaa,Rafiki amekwenda kupima na kugundulika ana TB nao waende wakafanyiwe vipimo mapema kwani kuna huduma ya kinga au matibabu mapema kabla ugonjwa haujawa sugu”amesema Dkt Seif
Dkt Seif Ameendelea kusisitiza kuwa kuugua TB siyo kufa inatibika kabisa kwani mtu yeyote asisubiri kufika kituo cha Afya akiwa amechelewa kwani gharama zake ziko tofauti TB ya kwanza ikigundulika haina vimelea vingi gharama yake ni laki 6 TB Kawaida sugu Milioni 32 na Sugu kabisa daraja la tatu Milioni 64 gharama zote hizo hulipwa na serikali hivyo ni vyema kuwahi vituo vya kutolea huduma mapema kwani TB hutibika kati ya miezi 6-12 na TB sugu miezi 9-20
Naye Mratibu Kifua kikuu Mnazi Mmoja Dkt Linda Mutasa amesema kuwa kumekuwa na dhana iliyoenea kwenye jamii kuwa ugonjwa wa Kifua kikuu ukihusishwa na mila potofu kuwa ni wa kurithi kutoka kizazi hadi kizazi au ukihusishwa na ushirikina kuwa mtu amelogwa hivyo kupelekea watu wengi wasio na elimu kutofika vituo vya Afya au kufika kwa kuchelewa na wengine hupona na wengine hupoteza maisha kutokana na kuchelewa matibabu hivyo Jamii ielimishwe kuhusiana na Kifua kikuu.
“Na sisi Wahudumu wa afya tunakutana na changamoto ya wagonjwa ambao hawamalizi dawa hivyo hulazimika kuwasimamia wanywe dawa tukiwa tunawaona kutokana na baadhi yao wakipatiwa dawa wakianza kupata nafuu huacha dozi hivyo wanaporudi hospitali hutulazimu kutumia njia hiyo kusaidia janga hili la ugonjwa wa TB kupungua na maambikizi yake”amesema Dkt Linda
Kwa upande wake Dkt. Nelson Telekela kutoka Shirika la Tanzania (STOP Tb Partnership )Muungano wa Wadau wa kupambana dhidi ya Kifua Kikuu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Or-Tamisemi amesema wanamatarajio makubwa na Waandishi wa habari kuelimisha Umma kupitia mitandao ya Jamii,Magazeti,vipindi vya redio na TV kwa utoaji wa elimu kutoa taarifa sahihi za ugonjwa huo kwa wananchi.
Aidha kila mwaka hufanyima Maadhimisho ya Kifua kikuu Machi 24 mwaka na kilele chake itakuwa Mkoani Simiyu huku Mgeni Rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kuelekea siku hiyo jumbe mbalimbali zitatembea ikiwemo “Ndiyo tunaweza kutokomeza TB” “Yes we can end TB” World TBDay 2023.