Home Kitaifa JINSI KIJANA WA SIMIYU ALIVYOSHINDA MILIONI TANO ZA MAGIFTI DABO DABO

JINSI KIJANA WA SIMIYU ALIVYOSHINDA MILIONI TANO ZA MAGIFTI DABO DABO

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Joseph Mutalemwa(kushoto) akizungumza na mshindi wa Magifti Dabodabo Shilingi milioni tano mkazi wa Kidinda mkoa Simiyu Robin Brasio, alipomtembelea kwenye duka lake la spea za pikipiki eneo la njia panda ya Ngulyani mjini Bariadi, baada ya kumkabidhi hundi yake, kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Simiyu.

Na Mwandishi wetu

Kampuni ya huduma za mawasiliano ya Tigo imekabidhi kiasi cha Shilingi Milioni Tano kwa Robin Brasio ambaye ni mkazi wa eneo la Kidinda na miliki wa duka la spea za pikipiki wilayani Bariadi mkoani Simiyu, baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni ya Magifti Dabodabo.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika  eneo la njiapanda ya Ngulyati mjini hapa Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Joseph Mutalemwa amewakumbusha wakazi wa Bariadi  na nchi nzima kuendelea kutumia huduma mbalimbali za mtandao huo mara kwa mara ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi.

“Mtandao wenu wa Tigo unawapenda na kuwajali sana, mnachotakiwa kufanya ni kufanya miamala na kujiunga na vifurushi kila wakati ambapo utabahatika kujishindia zawadi mbalimbali hata ile zawadi kubwa ya magari mawili, ambapo moja utampa umpendaye” amesema Mutalemwa.

Naye Diwani wa kata ya Bariadi Kija Bulenya akaishukuru kampuni ya Tigo kwa kumpatia zawadi kijana wa Bariadi ambapo kwake imekuwa mara ya kwanza kushuhudia mshindi akipewa zawadi.

“Ni furaha ilioje kwangu kuona mkazi wa hapa Bariadi akipewa pesa alizoshinda, huwa nasikia tu matangazo ya Magifti Dabodabo kwenye Runinga na Radio, nichukue fursa hii kwahamasisha wakazi wa Bariadi na nchi nzima kuendendelea kutumia huduma za Tigo kwa wingi” amesema Bulenya.

Kwa upande wake mshindi wa Magifti Dabodabo Robin  Brasio ameishukuru Tigo kwa kumpatia kiasi hicho cha pesa na kusema atazitumia vizuri ili zilete tija maishani.

“Nitanunua bodaboda moja na kuifanya ya biashara ili iniingizie kipato, pesa zitakazobaki nitaongeza spea za pikipiki hapa katika duka langu ili niuze na kupata faida. amesema Brasio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!