Home Kitaifa JESHI LA POLISI NCHINI LARIDHISHWA NA HALI YA USALAMA NA UTULIVU MKOA...

JESHI LA POLISI NCHINI LARIDHISHWA NA HALI YA USALAMA NA UTULIVU MKOA WA MARA

Na Shomari Binda- Musoma

JESHI la Polisi Nchini limeiridhishwa na hali ya ulinzi na usalama uliopo kwa sasa mkoani Mara huku wananchi wakiendelea kufanya shughuli za maendeleo bila wasiwasi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mara ambaye pia ni mkuu wa mkoa huo,Said Mtanda, mara baada ya kufanya mazungumzo mafupi na Mkuu wa jeshi la polisi nchini ( IGP) Camilius Wambura, alipomtembelea ofisini kwake.

Amesema katika tathimini fupi waliyoifanya inaonyesha hali ya usalama ni nzuri tofauti na kipindi cha nyuma ambapo kumekuwa na matukio ya hapa na pale.

Mtanda amesema moja ya tukio lililotokea kipindi cha nyuma ni pamoja na kuuwawa kwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wilayani Butiama ambapo watuhumiwa wa tukio hilo walikamatwa.

Amesema baada ya tukio hilo hakuna taarifa kubwa za kutokuwepo kwa hali nzuri za usalama wa raia na mali zao na kazi zinaendelea.

Afande IGP amenitembelea ofisini na tumekuwa na mazungumzo mafupi kutathimini hali ya usalama ya mkoa wa Mara.

Tumejiridhisha hali ya usalama ni nzuri kwenye mkoa wa Mara ikiwa ni pamoja na kwenye kanda maalumu ya kipolisi ya Tarime na Rorya” amesema Mtanda.

Mkuu huyo wa mkoa amesema zipo changamoto za utendaji kazi kwa upande wa jeshi la polisi ikiwemo usafiri ambapo amedai (IGP) Camilius Wambura ameahidi wiki kuipa gari moja jeshi la polisi mkoa wa Mara wiki hii.

Aidha Mtanda amesema mkuu huyo wa jeshi la polisi nchini ameahidi pia katika kipindi cha mwezi mmoja gari lingine litatolewa kwaajili ya kanda maalumu ya Tarime na Rorya kwaajili ya kuimalisha ulinzi na usalama

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!