Jeshi la polisi mkoani Mwanza limezindua wiki ya nenda kwa usalama barabarani zoezi la uwekaji stika kwenye magari, bajaji na pikipiki ambao umefanywa katika viwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza ambapo kwa magari binafsi yatalipa shilingi elfu tano, ya biashara yatalipa shilingi elfu saba, pikipiki na bajaji shilingi elfu mbili
Kamanda Mutafungwa amesema, wiki ya nenda kwa usalama kitaifa itafanyika jijini Mwanza ambapo kwa kipindi hicho askari polisi kitengo cha usalama barabarani watatoa elimu ya usalama barabarani na madereva kuzingatia elimu ya usalama barabarani watakayopewa kabla ya kupewa stika
Kamanda Mutafungwa amebainisha maeneo ya ukaguzi, ni eneo la nanenane, furahisha, buhongwa shule ya msingi na vituo vyote vya mabasi yaendayo nje na ndani ya mkoa huku akisema stika hizo zitauzwa kati ya shilingi elfu tano binafsi, biashara 7, pikpiki na bajaji elfu mbili.