Home Kitaifa JESHI LA POLISI MOROGORO LAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA...

JESHI LA POLISI MOROGORO LAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MKEWE

JESHI la Polisi mkoani Morogoro  linamshikilia mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la  Mohamedi Omari  mkazi wa kijiji cha Kimamba A wilayani  Kilosa  kwa tuhuma za  kumuua mkewe  na kumzika ndani ya chumba chao.

Mohamedi Omari mkazi wa kijiji cha Kimamba A  wilayani Kilosa mkoani Morogoro kamuua mkewe na kisha kumzika ndani ya chumba wanacho lala limeonekana kushangaza wengi.

Ni tukio la kuhuzunisha  tukio ambalo kabla ya kifo chake inadaiwa  baada ya kipigo kikali  kutoka kwa mumewe huyo mama alilia kwa uchungu akimsisitiza kutunza watoto wake ambao hakuzaa nae.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa baada ya kufanya mahojiano na watoto wa mama huyo aliyetambulika kwa jina la Beatrice Haiyasi wameeleza jinsi walivyopitia unyanyasaji mpaka kupelekea kukosa huduma muhimu za kielimu kutokana na kufungiwa ndani.

Pia ameeleza kuwa tukio hilo limebainika mara baada ya mtuhumiwa huyo kudaiwa kuuza mabati ya mwanamke wake ambaye amekuwa akiishi nae baada ya kumuua Beatrice ndipo kukatokea ugomvi na baadae watoto wa marehemu wakawa wanamkanya mama huyo asigombane na mtuhumiwa kwani atamuua kama alivyomuua mama yao.

Tulipata taarifa za mama huyu kuuawa na mume wake kutoka kwa wasamaria wema hii ni baada ya kutokea ugomvi kati ya mtuhumiwa na mke wake wa sasa ndipo watoto wa marehemu wakaanza kumkanya mama huyo kuwa asigombane na mtuhumiwa huyo kwani atauawa kama alivyouawa mama yao ndipo mama huyo akatoa taarifa kwa mamlaka husika,” amesema DC Shaka.

Kwa upande wao majirani wameeleza kuwa familia hiyo ilikuwa ni ngeni katika eneo hilo hawakuwa wanachangamana na wakazi wa eneo hilo kwani walikuwa ni watu wa kujifungia ndani.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema tayari wamemshikilia mtuhumiwa huyo kwa uchunguzi zaidi na uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!