Home Kitaifa JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LAPIGA MARUFUKU DISCO TOTO

JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LAPIGA MARUFUKU DISCO TOTO

Katika kuelekea Sikukuu za Mwisho wa Mwaka Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limepiga marufuku Disco toto katika kusherehea Sikukuu ya Mwaka Mpya na Christmas huku likitoa wito kwa Wazazi na Walezi kuhakikisha watoto awaendi kwenye madisco ambayo yanaweza kuleta msongano na kusababisha madhara kwa watoto.

Agizo hilo limetolewa na Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Mwanza Kamishina Mwandamizi Msaidizi Wilbord Mutafungwa wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linawataka watumiaji wote wa barabara ikiwa ni watembea kwa miguu,wapanda baiskeli,wasukuma guta na wanaotumia vyombo vya moto kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe anafuata sheria za usalama barabarani ili kuweza kuzuia ajali zinazoweza kuepukika

Katika hatua Nyingine Kamanda Mtafungwa ameitaka jamii ibadilike na kuachana na dhana potofu iliyojengeka kwa mwisho wa mwaka huwa na matukio mabaya yakihusisha vifo,uhalifu ,mikosi na ajali za barabarani badala yake wachukulie kawaida na waamini kuwa ni kipindi kama vilivyo vipindi vingine na waishi kwa kufuata sheria .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!