Home Kitaifa JESHI LA POLISI MKOA WA PWANI LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA 354 KATIKA MWEZI AGOSTI

JESHI LA POLISI MKOA WA PWANI LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA 354 KATIKA MWEZI AGOSTI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watuhumiwa 354 waliohusika katika uhalifu wa makosa mbalimbali ya jinai ikiwa ni pamoja na kukamata nyama ya swala na magamba 11 ya kakakuona ambazo ni nyara za serikali katika mwezi agosti mwaka huu .

Akizungumza na waandishi wa habari mjini kibaha ofisini kwake kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Muhudhwari R. Msuya amesema jeshi hilo limefanya misako na operesheni mbalimbali kwa lengo la kuzuia na kutanzua uhalifu kuanzia tarehe 01/08/2023 hadi 31/08/2023 na kufanikiwa kukamata watuhumiwa hao 354.

ACP Msuya amesema kwa upande wa waliokamatwa na nyara za hizo za serikali jeshi hilo kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori limefanikiwa kukamata nyama ya swala na magamba 11 ya kakakuona na watuhumiwa 14 wamekatwa kati yao 03 wamefikishwa mahakamani.

Amesema watuhumiwa 114 wamekamatwa katika makosa ya kupatikana na dawa zinazodhaniwa kuwa ni zakulevya ikiwa ni pamoja na Bhangi viroba 7, Puri 60, Kete 791 na Mbegu za Bangi kg 5, Mirungi Kilo 5, Bunda 3 za mirungi.

Wengine watuhumiwa 4 wamekamatwa kwa makosa ya kubaka na 6 kwa makosa ya uvunjaji na watuhumiwa 99 wamekamatwa kwa tuhuma za makosa ya pombe haramu ya moshi “gongo” lita 368 na mitambo miwili ya kutengeneza pombe ya moshi.

Amesema pia Jeshi hilo la Polisi pia limekamata watuhumiwa 97 kwajumla ya Pikipiki aina mbalimbali 111 aina tofauti tofauti zidhaniwazo kuwa za wizi.

Watuhumiwa 5 wamekamatwa kwa tuhuma za mali za wizi wa Ngombe 02 na Mbuzi 03 mali za wizi, Wahamiaji haramu 03 toka nchi ya Ethiopia 01, Kenya 01 na Uganda 01 ambao wamefikishwa idara ya Uhamiaji kwa hatua za kisheria.Aidha mtuhumiwa 1 anashikiriwa kwa kukamatwa na Mafuta ya kupikia madumu 05 aina ya mico gold na mtuhumiwa 01 ambaye alifikishwa TRA kwa hatua za kisheria na watuhumiwa 28 wamekamatwa na mali mbalimbali zilizoibiwa katika matukio ya wizi na uvunjaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!