Home Kitaifa JESHI LA POLISI MKOA WA MARA LAWATAHADHALISHA WAHALIFU SHEREHE ZA PASAKA

JESHI LA POLISI MKOA WA MARA LAWATAHADHALISHA WAHALIFU SHEREHE ZA PASAKA

Na Shomari Binda-Musoma

JESHI la polisi mkoa wa Mara limewatahadhalisha wale wote watakaofanya vitendo vya uharifu wakati wa sherehe za sikukuu ya Pasaka.

Tahadhali hiyo imetolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Mara Salim Morcase alipozungumza na Mzawa Blog kuelekea sherehe hizo.

Amesema wamejipanga kuimarisha masuala ya usalama ili wananchi waweze kusherehekea sherehe hizo kwa amani na usalama.

Kamanda huyo amesema mtu au watu watakaopanga kufanya vitendo vya uhalifu kwenye sherehe hizo wataishia mikononi mwa polisi.

Amesema askari wapo tayari kuhakikisha ulinzi unaimalishwa ikiwa ni kwenye nyumba za ibada na maeneo mengine ili usalama uwepo.

Ametoa rai pia kwa wananchi ambapo wanapaswa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kupitia polisi Kata ili kwa pamoja kuweza kudhibiti uhalifu.

Jeshi la polisi mkoa wa Mara linatoa tahadhali kwa mtu au watu watakaotaka kufanya vitendo vya uhalifu. Askari wapo tayari kwa doria za aina mbalimbali kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu ya Pasaka kwa amani” amesema

Aidha kamanda Morcase amewataka madereva wa vyombo vya moto kuendesha kwa tahadhali ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza kupelekea majeruhi na vifo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!