Home Michezo JESHI LA POLISI LATOA TAHADHARI MECHI YA SIMBA NA AL AHLY

JESHI LA POLISI LATOA TAHADHARI MECHI YA SIMBA NA AL AHLY

Na. Magrethy Katengu

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam limewataka mashabiki watakaohudhuria kwenye mechi ya Simba sc na Al Ahly itakayofanyika oktoba 20 mwaka huu katika uzinduzi Machindano ya Afrika katika uwanja wa Benjamin Mkapa kutokwenda na watoto wadogo bila kuwakatia tiketi kwenye mchezo huo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaaam mara baada ya kutoka katika uwanja huo kuhakikisha usalama, Kamanda wa kanda hiyo Jumanne Muliro kumekuwa na matukio ya watoto kuzagaa na kuwabugudhi mashabiki kutokana na wazazi wao kwenda nao uwanjani bila kuwakatia tiketi jambo ambalo limekuwa ni kero.

Kutakuwa na mchezo wa soka hatua ya robo fainali ya mashindano hayo baina ya klabu ya Simba ya Tanzania na Al Ahly ya nchini Misri utakaochezwa kuanzia majira ya saa 12:00 jioni, ambapo mifumo ya Usalama imeimarishwa.

SACP Muliro amesema kuwa, jeshi la Polisi linatambua mchezo huo utahusisha wageni
kutoka nje ya nchi na kuwa na mkusanyiko mkubwa katika Kiwanja hicho, kutokana na hali hiyo baadhi ya barabara zitafungwa ili kupunguza msongamano wa kuelekea uwanjani hapo, hivyo mashabiki wa soka wafike mapema ili kuepukaa usumbufu unaoweza kuepukika.

“Jeshi la Polisi limechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo, ukaguzi wa hali ya juu katika mageti ya kuingia na hairuhisiwa mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa baadhi ya vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo” amesema

Ameongeza kuwa mtu yoyote asiyekuwa na tiketi hataruhusiwa kusogelea uwanja huo au maeneo ya milango ya kuingia ili usalama uimarishwe zaidi kutokana na uhalisia wa kuwepo kwa watu wengi uwanjani hapo.

SACP Muliro ameongeza kuwa jeshi la polisi halitavumilia tabia hizo na zingine ambazo
zimepigwa marufuku na vyama vya soka FIFA, CAF na TFF tabia ambazo zinaweza kupelekea Tanzania kukosa sifa ya kuandaa mashindano kama haya wakati mwingine.

“Watakao kaidi, watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria, Jeshi la Polisi linawataka mashabiki wa soka kushangilia kistaarabu nakuacha alama nzuri ya kiusalama Katika Taifa la Tanzania” amesisitiza kwenye Mkutano huo na Waandishi wa habari.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam
limewatahadharisha baadhi ya mashabiki wenye tabia ya kuwasha fataki au baruti uwanjani, na kwamba atakayefanya hivo kisheria kali zitachukuliwa hatua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!