Home Kitaifa JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WAJIPANGA KUDHIBITI AJALI

JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WAJIPANGA KUDHIBITI AJALI

Na Magreth Mbinga

Jeshi la Polisi kikosi Cha usalama barabarani kimehakikisha kinadhibiti ajali za barabarani zinazotokea hususa ni nyakati za usiku na kusababisha vifo vya watu na majeruhi.

Amesema hayo Jijini Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa kikosi Cha usalama barabarani SACP Ramadhani Ng’anzi wakati akizindua operesheni ya ukaguzi wa vyombo vya moto ikiwemo magari,pikipiki na bajaji Nchi nzima ambapo watakagua leseni za madereva ,stika na ubora wa chombo.

“Katika tathimini yetu tumegundua kuwa ajali nyingi zinazosababisha vifo hutokea wakati wa usiku asilimia kubwa magari ya kubeba mizigo kugongana na magari ya abiria na gari binafsi hivo operesheni yetu kabambe itafanyika muda wote”amesema SACP Ng’anzi.

Pia Ng’anzi amesema lengo la kufanya ukaguzi wa magari hayo ni kuona kwamba vyombo vyote vinavyotumika barabarani ni Salama wanapima umadhubuti wa gari kwa vigezo na mifumo yote ya magari kuanzia breki,mfumo wa umeme na ametoa maagizo kwa RTO wote Nchi nzima watege maeneo Maalum ya ukaguzi wa magari na litaanza Leo tarehe 6 mwezi wa tatu hadi tarehe 13 mwezi wa 3 siku ya sherehe za usalama barabarani.

“Wiki ya usalama barabarani inatanguliwa na ukaguzi wa magari na utoaji wa elimu kwa watumiaji wa barabara kwahiyo matarajio yangu madereva wote kuanzia yanayobeba abiria,mizigo ,magari ya mafuta ,magari yanayobeba wanafunzi yaliyokaguliwa hivi karibuni,pikipiki,bajaji wanaweza kufika katika kituo cha Polisi kwaajili ya ukaguzi na Jeshi la Polisi litatoa hati maalumu kuonyesha kwamba chombo hiko kimekaguliwa na inavigezo vya kuingia barabarani “amesema SACP Ng’anzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Bima kutoka Benki ya NMB Martini Masawe amesema Benki hiyo imetoa udhamini katika Operesheni Kabambe kwa kuwa wanaguswa na ajali zinazotokea hivyo wataendelea kuunga mkono suala hilo ili kusaidia ajali zinapungua kabisa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!