Home Kitaifa JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MWANAFUNZI NA KUMSABABISHIA UJAUZITO

JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MWANAFUNZI NA KUMSABABISHIA UJAUZITO

Na Shomari Binda-Simiyu

MAHAKAMA ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela na faini ya shilingi 300,000 Jeri Msalenge mwenye umri wa miaka 20 kwa kumbaka mwanafunzi na kumsababishia ujauzito.

Hukumu hiyo imetolewa kutokana na shauri la jinai Na.50/2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Itilima mbele ya Hakimu Mkazi Roberth Kaanwa.

Mshitakiwa hiyo mkazi wa Sagata Itilima alishitakiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Itilima kwa kosa la kubaka kinyume na kifungu cha 130(1)(2)e na 131(1) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2022.

Awali Mahakamani hapo ilidaiwa na mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya taifa ya mashtaka wilaya ya Itilima Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Vedastus Wajanga kuwa mshitakiwa akiwa katika Kijiji cha Sagata akiwa anachunga ng’ombe kwa ndugu yake mnamo tarehe 15/06/2023 na trh 28/06/2023 huko Kijiji cha Sagata ndani ya wilaya Itilima alimbaka mhanga mwenye umri wa Miaka 16 mwanafunzi wa kidato cha pili na kumsababishia maumivu pamoja na ujauzito.

Imedaiwa taarifa zilifika kituo cha polisi tarehe 04/09/2023 na tarehe 18/09/2023 alifikishwa Mahakamani na kusomewa kosa lake.

Jumla ya mashahidi wanne na kielelezo kimoja kilitolewa na upande wa mashtaka.
baada ya ushahidi huo mshtakiwa alijitetea mwenyewe na Mahakama ya wilaya ya Itilima ilimtia hatiani mshitakiwa kwa kosa la kubaka kifungu 130(1),(2)e na 131 (1) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2022.

Baada ya kutiwa hatiani upande wa mashtaka uliomba apewe adhabu kali ili iwe funzo kwake na kwa jamii kwani matukio kama hayo huacha kumbukumbu mbaya isiyo futika kirahisi katika maisha ya mhanga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa na muhanga anaujauzito na mtoto anazaa mtoto mwenzake.

Mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na Hakimu Roberth Kaanwa kutoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela na fidia ya shilingi 300,000 na kutoa haki ya rufaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!