Home Kitaifa JAMII YAASWA KUTENDA MEMA

JAMII YAASWA KUTENDA MEMA

JAMII imeaswa kutenda matendo mema ili kudumisha misingi ya utulivu ambayo taifa letu imejenga kwa muda mrefu.

Wito huo umetolewa kwa nyakati tofauti jana Jijini Mwanza na viongozi wa madhebu mbalimbali ya dini ya kiislamu katika sherehe za Eid Elftri.

Shehe Yahya Ali wa Al-Asasy Makongoro alisema mfungo waliyofanya ilikuwa kama chuo kwao kuweza kutafakari juu ya yale Mungu anataka wanadamu kutenda hapa duniani.

Alisema wanamwombea Rais kwa Mungu amlinde ili aweze kuendeleza yale mema yanayopashwa kufanywa kwa watanzania wote.

Shehe Sululu Salum wa Masjid Kirumba aliwataka watanzania kudumisha upendo na ushirikiano ili taifa liweze kupiga hatua za kimaendeleo.

Alisema maovu yaliyopo kwenye jamii kama vile ukatilli wa kijinsia na kwa watoto haina budi kukomeshwa kwani inaleta ghadhabu kwa Mungu.

Naye Imam wa Msikiti waTaqwa Abdul Muhammad alisema mfungo waliyofanya umeweza kuwajenga kiimani na hivyo kuwafanya kushukuru namna Mungu alivyo na upendo mkubwa kwa wanadamu.

Kuna watu ambao walikuwa na matendo maovu ndani ya Jamii hata hivyo kutokana na upendo wa Mungu wamebadilika na hivyo kufuata mambo mazuri”alisema Imam Muhammad.

Alisema thamani ya mtu ni pale anapomjua Mungu na kuyafanya ya kumpendeza ambayo ni kujitenga na maovu yote kwenye jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!