Na Shomari Binda-Musoma
WANANCHI jamii wanaotoka Musoma na kuishi maeneo mbalimbali nchini wanatarajiwa kukutana februari mosi mjini Musoma kujadili maendeleo.
Katibu wa wana jamii hao ambao umoja huo ulianzishwa kupitia group la whasap Gedion Webi amesema tangu kuanzishwa kwake kumekuwa na mafanikio na kukutana kutaongeza mafanikio.
Webi amesema kila mwisho wa mwaka wamekuwa wakikutana na kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kusaidiana wakati wa matatizo.
Katibu huyo amesema mpaka sasa wamefanikiwa kwenye eneo la kusaidiana hasa wakati wa mmoja wapo anapopatwa na msiba na wana jamii wamekuwa wakiitikia kuchanga.
Amesema wanataka kufikia mbali zaidi kupitia umoja huo hasa kwenye masuala ya maendeleo ikiwemo kuinuana kiuchumi.
Webi amesema ili kufanikisha kukutana kila mwana jamii anapaswa kuchangia kama ambavyo michango inaendelea.
” Nawashukuru wana jamii wote ambao wanaendelea kuchangia ili tuweze kukutana na kujadili mambo yetu.
” Umoja wa jamii ya wana Musoma imekuwa na mafanikio na kupitia Mwenyekiti wetu Magiri Benedict tunataka kufika mbali zaidi”,amesema.
Baadhi ya wana jamii wa Musoma waliopata kusaidiwa na umoja huo wamesema ni moja ya umoja ambao unapaswa kusonga mbele kutokana na manufaa yake.