Mwenyekiti wa Chama chetu Rais Dkt Samia Suluhu HAssan ameruhusu mikutano ya hadhara sisi kama chama tuko tayari tutaenda kuwajibu wapinzani kwa hoja kutokana na miradi inayotekelezwa na mwenyekiti wa chama chetu, Dkt Samia, Jamal Babu mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Mkoa wa Mwanza, MNEC.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa, mkoa wa Mwanza Jamal Babu ameshiriki zoezi la upandaji miti katika shule ya sekondari Buzuruga ikiwa ni kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa chama hicho.
Aidha, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza Jamal Babu, amemuomba Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuhakikisha mradi wa tenki la maji liliopo katika eneo la Buswelu Manispaa ya Ilemela unakamilika kutokana na wakazi wa maeneo hayo kuishi pembezoni mwa ziwa Victoria na wakiendelea kukosa huduma hiyo muhimu.
Diwani wa kata ya Buzuruga na naibu meya wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza Manusura Sadiki amempongeza Rais Dkt. Samia Suruhu Hassan pamoja na mbunge wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Buzuruga