Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo ameongoza matembezi ya hisani pamoja na Uzinduzi wa Kampeni ya STAMICO na Mazingira At 50 iliyofanyika leo Agosti 11, 2022 Jijini Dodoma
Hafla hiyo imehudhuliwa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse, Watendaji wa Wizara na Taasisi zake pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini na Mazingira.
Matukio hayo yametanguliwa na mazoezi ya viungo yaliyoongozwa na wataalam wabobezi.