Home Biashara JAFO AAGIZA UKAGUZI WA MAKAMPUNI YA KIGENI YALIYOUNGANA NA KAMPUNI ZA NDANI

JAFO AAGIZA UKAGUZI WA MAKAMPUNI YA KIGENI YALIYOUNGANA NA KAMPUNI ZA NDANI

Na Ritha Jacob – Dar es salaam

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Seleman Jafo, ameagiza Tume ya Ushindani (FCC) kufanya ukaguzi wa kampuni za kigeni zilizoungana kibiashara na kampuni za ndani ili kubaini kama zinafanya biashara kwa misingi ya sheria na ushindani unaokubalika sokoni.

Akizungumza na uongozi wa Tume hiyo jijini Dar es Salaam tarehe 12 Agosti 2024, Jafo alisisitiza umuhimu wa FCC kutembelea maeneo ya uchimbaji wa madini na makampuni yanayohusika na madini nchini ili kuangalia kama usawa na sheria zinafuatwa, kwani eneo hili limekuwa likiwakandamiza wachimbaji wadogo kwa makampuni makubwa kununua hisa zote bila kufuata sheria, hivyo kuipotezea serikali mapato.

Serikali inatambua mchango wa kampuni za kigeni kuingia ubia na kampuni za ndani katika kuchangia pato la serikali, lakini bado kuna haja ya kufanya ukaguzi kubaini kama zinafanya kazi inayoendana na sheria ya ushindani,” alisema Jafo.

Pia, Jafo alihimiza FCC kutoa elimu kwa wananchi, wamiliki wadogo wa viwanda, na wa viwanda vikubwa, pamoja na kuwakaribisha wawekezaji kutoka nje ya nchi kuja kufanya uwekezaji kwa kufuata sheria. Kwa kufanya hivyo, Serikali itaweza kuingiza fedha nyingi kwa manufaa ya Watanzania.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, William Erio, amesema tume hiyo inaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kwa kuhakikisha mikataba wanayoingia haina changamoto zinazoweza kuathiri biashara zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!