Home Kitaifa INALIPA WAZINDUA PROGRAM AMBAYO ITAPUNGUZA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA

INALIPA WAZINDUA PROGRAM AMBAYO ITAPUNGUZA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA

Na Magreth Mbinga

Kampuni ya biashara ya mtandaoni ya Inalipa leo Novemba 21 ,2022 imezindua programu mpya ya kibunifu ya uza ambayo inatazamiwa kuwa chombo kinachohitajika sana kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana.

Akizungumza wakati wa uzinduzi Meneja mradi wa Inalipa Bertha Shao na kusema kuwa dira ya msingi ya Inalipa ni kuona Afrika ambayo inakampuni kubwa za bidhaa za walaji zinapata urahisi wa kusambaza bidhaa katika soko,kupata taarifa muhimu ambazo zitawasaidia kuwa na ufahamu mzuri wa wateja wao.

Leo Inalipa imezindua programu ya mauzo ambayo inaruhusu mtu yeyote kujiunga na kuwa bosi binafsi kwa kuuza bidhaa kwa jumla na inatoa zawadi za papo hapo kwa watumiaji wake ,ina ubao utakaoonyesha msimamo wa wanaoongoza wenye ushindani kwa wauzaji kupata zawadi na zaidi” amesema Shao.

Pia Shao amesema wanaamini katika nguvu ya vijana kuendesha maendeleo ya Tanzania na kuongoza katika siku za usoni kuna vijana milioni moja wanaohitimu na kuingia katika soko la ajira kila mwaka ambapo vijana hao wanauwezo wa ujasiriamali ila hawana usaidizi unaofaa kujiptia kipato Uza ni jibu katika hilo na wanaamini italeta mapinduzi katika sekta .

Aidha Balozi wa Uza Millard Ayo amesema njia ambayo wameitumia Inalipa ni chanya kwasababu itapunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana ambao wanatoka chuo.

Hawa Inalipa ambao wamekuja na zao la Uza nawafahamu kwa muda mrefu wakati wanaanza Inalipa walinishirikisha kwa uzuri na hii ya uza wamenishirikisha nimeona mchakato wao kuanzia mwanzo mpaka mwisho kwahiyo bidhaa hii Ni nzuri hakuna ujanja ujanja” amesema Millard.

Sanjari na hayo mmiliki wa simulizi na sauti na mjasiriamali katika maswala ya teknolojia Fredrick Bundala amesema Uza inakuja kuleta ukombosi mkubwa sana kwa vijana kwasababu inawswezesha vijana kujiajiri kwa kutafuta wateja na unapata malipo kulingana na wateja ambao umewaleta.

Uza inahusisha kusajiri maduka mbalimbali ambayo yanauza bidhaa kwa rejareja unapata kwa jumla kwa kutumia Uza unaketewa mzigo palepale ulipo “amesema Bundala.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!