Home Kitaifa IMF YAIDHINISHA MKOPO NAFUU WA DOLA MILIONI 153 KUSAIDIA BAJETI YA SERIKALI

IMF YAIDHINISHA MKOPO NAFUU WA DOLA MILIONI 153 KUSAIDIA BAJETI YA SERIKALI

Tafadhali tunaomba msaada

Na Joseph Mahumi, WFM

SHIRIKA la Fedha la Kimataifa (IMF), jana Jumatatu Aprili 24, 2023 limeidhinisha kutolewa kwa mkopo wenye masharti nafuu wa kiasi cha dola za kimarekani milioni 153 kwa ajili ya kusaidia bajeti ya Serikali ya Tanzania.

Akizungumzia Taarifa hiyo ya IMF, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Waizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja  ameeleza kuwa kuidhinishwa kwa kiasi hicho cha fedha kunafuatia Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo kuridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali zilizochangia nchi kuwa na uchumi madhubuti na kusimamia vizuri Deni lake la Taifa licha ya dunia kupitia changamoto za kiuchumi.

Uamuzi huo unafanya fedha zilizoidhinishwa na IMF kupatiwa Tanzania kufikia dola za Kimarekani milioni 305 kati ya mkopo ulioidhinishwa mwaka jana na Shirika hilo wa dola bilioni 1.4.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!