Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mzanva amewaagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuhakikisha wanapata hati miliki ya eneo waliloweka mradi wa maji katika Wilaya ya Gairo ili kunusuru madhara yanayoweza kujitokeza ikiwa eneo hilo halitakua na hati.
Â
Mradi huu wa maji ambao unaenda kulisha wakazi wa Makuyu na maeneo ya jirani hivyo kukidhi vigezo vya kuzinduliwa na mwenge wa uhuru kwa mwaka 2024 umegharimu zaidi ya shilingi milioni  513 aghalabu unaenda kuwa mwarobaini wa  changamoto ya maji hasa kutembea umbali mrefu kwa wakazi wa maeneo hayo.
Â
Baada ya kuzindua mradi huo, kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mzanva ametoa maagizo kwa wasimamizi ili uwe na tija iliyokusudiwa kuanzishwa kwake.