Home Kitaifa IEP YATOA MATOKEO WATAHINIWA WALIOFANYA MTIHANI WA DINI YA KIISLAM DARASA LA...

IEP YATOA MATOKEO WATAHINIWA WALIOFANYA MTIHANI WA DINI YA KIISLAM DARASA LA 7

Na Magrethy Katengu

Islamic Education Panel (IEP), imetoa matokeo ya watahiniwa waliofanya mtihani wa masomo ya dini ya Kiislamu na lugha ya Kiarabu kwa wanafunzi wa darasa la saba ambapo wamefaulu wanafunzi 139,181 sawa na asilimia 88.19 kati ya watahiniwa wote 157,823.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mjumbe jopo la IEP, Alhaji Sheikh Musa Kundecha amesema mtihani huo ulifanyika Agosti 9 mwaka huu, ambapo idadi ya watahiniwa wameongezeka kutoka 150,945 kwa mwaka 2022 hadi kufikia 157,823 kwa mwaka huu.

Aidha amesema jumla ya shule 3,975 katika mikoa 26 ya Tanzania bara na visiwa vya Unguja na Pemba walifanya mtihani huo na kuhusisha halmashauri 159 ambapo mtihani ulikuwa na alama 50 na matokeo yametolewa kwa madaraja ya A hadi E.

Sambamba na hayo amesema idadi ya shule zilizofanya mtihani huo umeongezeka kutoka 3903 kwa mwaka 2022 hadi kufikia 3975 sawa na asilimia 1.8 kwa mwaka huu na Halmashauri kutoka halmashauri 151 hadi kufikia halmashauri 158.

Hata hivyo amesema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa somo la elimu ya dini ya Kiislamu walikuwa 174,719 kati ya hao waliofanya walikuwa 157,823 sawa na asilimia 90.33.
Sheikh Kundecha amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa kupata daraja A hadi D ni 139,181 sawa na asilimia 88.19 na daraja E ni 18,591 sawa na asilimia 11.81 ya watahiniwa wote.
Ametaja shule kumi bora zilizopo katika halmashauri ambazo Temeke, Nachingwea, Mkuranga, Mwnza, Ilemela, Dodoma, Mafia, Kigamboni, Bukoba na Masasi na shule kumi za mwisho katika mtihani huo zimetoka katika halmashauri za Tabora, Same, Urambo, Kisarawe, Kilimanjaro na Mpanda.

Katika hatua nyingine amesema IEP imeendesha mtihani wa Kitaifa wa kuhitimu elimu ya madrasa ambayo imejumuisha masomo matatu ya maarifa ya uislamu, Quran na lugha ya Kiarabu.

Jumla ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 166, waliofanya mtihani ni 95 sawa na asilimia 57.23 na ambao hawakufanya ni kwa sababu mbalimbali ni 71 sawa na asilimia 42.77.

Hata hivyo ameeleza kuwa lengo ni kuratibu madrasa zote ziwepo kwenye mfumo zilizopo mtaani na madrasa zinapata changamoto wa mwingiliano wa mitihani ya shule.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!