Home Afya ICAP yatoa mashine na vifaa tiba vya zaidi ya milioni 110 mkoani...

ICAP yatoa mashine na vifaa tiba vya zaidi ya milioni 110 mkoani Mwanza

Na Neema Kandoro Mwanza

SHIRIKA LA ICAP Mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Mfuko wa Rais Marekani wa dharura katika kupambana na ukimwi (PEPFAR) imetoa mashine za upimaji saratai kwa shingo la uzazi na vifaa tiba kwa watu waishio na maambukizi ya virus vya Ukimwi vyenye thamani ya zaidi ya sh milioni 110.

Hayo yamebainishwa leo jijini hapa na Meneja wa ICAP mkoani hapa Dk Joseph Obeid akisema vifaa vilivyotolewa kuwa ni mashine 10 za uchunguzi was shingo la uzazi zenye thamani ya mikioni 100 ambazo zitatolewa kwa halmashauri ya Misungwi 2, Nyamagana 1, Ukerewe 2, Buchosa1,Sengerema 1, Ilemela 1, Kwimba 1 na Magu 1.

Alisema kuwa vifaa vingine kuwa ni vya elimu na burudani kwa ajili ya Kiliniki, vifaa vya matibabu ya saratani ya shingo la uzazi,vifaa vya kufubaza ukimwi na vya kinga ambavyo vina thamani ya milioni 10.

“Tumedhamiria kutokomeza matatizo hayo katika eneo hili kwa sasa kupitia mradi huu wa sasa” alisema Dk Obeid.

Dk Ibeid alisema kuwa vifaa hivyo vimetolewa kupitia mradi wa Fikia + katika halmashauri zote nane za mkoani Mwanza ili kupunguza na kuondoa matatizo hayo kwenye eneo hili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!