Home Kimataifa HUDUMA YA MAJI KATAVI KUPATIKANA KWA UHAKIKA-MHE.MARYPRISCA MAHUNDI

HUDUMA YA MAJI KATAVI KUPATIKANA KWA UHAKIKA-MHE.MARYPRISCA MAHUNDI

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi kuwa serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji ikiwemo bwawa la Senkwa ambalo linatarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya elfu 68.

Amesema ujenzi wa Bwawa hilo umefikia asilimia 80 na Serikali itahakikishia fedha za kukamilisha ujenzi huo zinapatikana kwa wakati ili kuhakikisha wananchi na akinamama wa Mlele wanatua ndoo ya maji kichwani.

Mhe. Maryprisca amewaahidi wananchi wa Katavi wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoni hapo.

Awali akitoa neno na ukaribisho kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Katavi, Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Isack Kamwelwe (Mb) amesema wananchi wa jimbo la Katavi wanaridhishwa na mwenendo wa Wizara ya Majj katika kuhakikisha huduma ya majisafi na salama inamfikia kila mwananchi. Amesema kwa sasa huduma hiyo ipo asilimia 78.

Amesema baada ya kukamilika kwa bwawa la Nsekwa na miradi mingine inayoendelea kutekelezwa jimboni hapo huduma ya maji itapatikana kwa zaidi ya asilimia 100.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!