Home Kitaifa HOTELI YA THANDA YA WILAYANI MAFIA YAPIGWA MARUFUKU KUCHOMA TAKA KWENYE HIFADHI...

HOTELI YA THANDA YA WILAYANI MAFIA YAPIGWA MARUFUKU KUCHOMA TAKA KWENYE HIFADHI YA BAHARI – NEMC

Baraza la Taifa la Huifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya mashariki kusini wapiga marufuku uchomaji taka katika hifadhi ya Bahari kwenye Hotel ya Thanda iliyowekeza kwenye Kisiwa cha Shungi mbili wilayani Mafia mkoani Pwani ilikulinda na kuhifadhi mazalia ya viumbe hai maeneo ya hifadhi ya Bahari.

Akizungumza wakati akiwa kwenye kisiwa cha Shungi mbili wilayani Mafia mkoani Pwani wakiwa kwenye mwendelezo wa ukaguzi wa kawaida wa kuangalia utekelezaji wa Sheria za mazingira na mashariti yanazotolewa kwenye vyeti wakati wa kupewa kibali cha NEMC kabla ya uanzishwaji wa hotei nchini.

Meneja wa NEMC Kanda ya mashariki kusini Lilian Kapakala amesema wamekuwa wakiangalia namna ambavyo Sheria ya mazingira ya mwaka 2004 inavyotekeleza na wawekezaji mbalimbali wakiwemo wenye viwanda na hoteli nchini.

Lilian amesema katika hoteli ya Thanda wamekuta wanachoma takataka jambo ambalo sio sahihi katika maeneo yaliyohifadhiwa “Hairuhusiwi kuchoma takataka kwenye mazingira na maeneo ya hifadhi ya Bahari kwani ni eneo la hifadhi ya Bahari bali chochote kinachoingia baada ya matumizi kinatakiwa kiondoke ndani ya hifadhi baada ya matumizi”

Alisema wawekezaji wote kwenye maeneo ya hifadhi ya Bahari na nje ya hifadhi ya Bahari wanatakiwa kuwa na eneo maalumu la hifadhi madhubuti ya kuhifadhi taka hatarishi kwenye maeneo yao ilikutunza na kuhifadhi mazingira nchini kama inavyoelekeza kwenye kanuni ya taka hatarishi ya uhifadhi na udhibiti wa taka hatarishi ya mwaka 2021.

Amesema agizo hilo ni kwa Hoteli zote zilizo katika maeneo hifadhi kwamba wasichome takataka zao bali waziondoe ndani ya hifadhi na alivitaja baadhi ya taka hizo kuwa ni pamoja na taka za vyombo vya kuhifadhi mafuta ya dizeli, vyuma, ndoo na makopo ya rangi, mabati yaliyotumika badala ya kuacha kwenye mazingira.

Amesema tunahitaji kuwa wa kweli katika kutunza mazingira yetu kwa kuzingatia namna ya kuhifadhi na kutunza taka na kuhakikisha taka zinahifadhiwa sawa na kanuni na Sheria za mazingira ya mwaka 2004.

Aidha Meneja huyo wa NEMC Kanda ya mashariki kusini alisisitiza wamiliki wa hoteli nchini kulipa ada na tozo za mazingira kwa wakati bila shuruti kila ifikapo mwaka mpya wa fedha wa serikali yaani tarehe 1 mwezi julai.

Hata hivyo NEMC wamesisitiza wamiliki wa wawekezaji kuzingatia mashariti waliyopewa kwenye cheti cha mazingira na sambamba ikiwa ni pamoja na kufanya Ukaguzi wa kimazingira sawa na takwa la sheria la kimazingira Kila mwaka na kulipa ada ya mazingira kwa muktaza wa kanuni za ada na tozo ya mwaka 2021

Akizungumzia tafadhali ya kuendeleza maeneo ya uwekezaji nchini Meneja huyo ameonya wenye Hoteli nchini kutoingiza chochote nchini wala kuendeleza wekezaji kwenye maeneo yao bila kibali kutoka NEMC na kuwataka kutoa taarifa za changamoto walizonazo kwenye Ofisi za Kanda za NEMC zilizo kwenye maeneo yao iliwashauriwe nini chakufanya sawa na mazingira ya maeneo yao husika.

Kwa upande wa matumizi nishati safi ya kupikia Lilian alisema kwenye mahoteli zote nchini wanatakiwa kutumia nishati safi ya kupikia na sio kutumia Kuni na mkaa ilikuendeleza uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Alisema NEMC ina ungana na Championi wa kwanza wa kutunza mazingira Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuhimiza matumizi ya nishati safi kwenye Hoteli zote nchini

NEMC Kanda ya mashariki kusini katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2023/24 na mwaka fedha wa 2024/25 wamekwisha tembelea na kukagua viwanda na Hoteli 150 zilizo katika hifadhi ya Bahari na zilizo nje ya hifadhi ya Bahari.

Mhifadhi Bahari wa Marine Park wa Wilaya ya Mafia Kulwa Mtaki alisema uchomaji taka kwenye mchanga ndani ya hifadhi ya Bahari ni kuua viumbe hai kwenye mchanga.

Wahifadhi wa Bahari haturuhusu kuchoma taka bali zinatakiwa zikusanywe na kupelekwa kwenye dampo kwaajili ya kurejerezwa, hata mmeenda kinyume na taratibu siku nyingine zikusanywe na kupeleka zilikoelekezwa na serikali” alisema Kulwa.

Mhasibu wa Thanda hoteli Tanzania limited Frank Philips alisema katika zoezi la utunzaji wa mazingira wanatumia mbinu zote mbadala kwaajili ya kuweka mazingira safi kwa kutumia mzabuni maalumu kwaajili ya kukusanya takataka na zinasafirishwa kwenda Dar es salaam kwa warejereshaji maalumu kabisa kwaajili ya rejeresha takataka

Na wala hatutumii plastiki kwenye maeneo yetu kwakuwa sisi tupo kwenye maeneo ya hifadhi ya Bahari” alisema.

Tunafanya juhudi kubwa ilikuweka mazingira yetu safi na salama kwaajili yetu sisi tunaoishi hapa na viumbe hai vinavyotuzunguka katika hifadhi hii ya Bahari” alisema Frank

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!