Home Kitaifa HOSPITAL YA MWALIMU NYERERE YATAJWA ENEO LA USALAMA WA TAIFA KWA KULINDA...

HOSPITAL YA MWALIMU NYERERE YATAJWA ENEO LA USALAMA WA TAIFA KWA KULINDA AFYA ZA WANANCHI

Na Shomari Binda-Musoma

HOSPITAL ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Musoma imetajwa kama eneo la Usalama wa Taifa kwa kulinda afya za wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi ” NDC” Meja Jenerali Willbert Augustine wakati wa ziara ya kuitembelea hospital hiyo.

Amesema tangu kuanza kujengwa kwa hospital mwaka 1975 kuanzia serikali ya awamu ya kwanza hadi ya sita ni kutoa huduma za afya kwa wananchi.

Meja Jenerali Augustine amesema kuwa na afya bora ni sehemu ya ulinzi wa taifa na kupongeza serikali kwa kuendelea kutenga fedha kwaajili ya ukamilishaji wa hospital hiyo.

Mkuu huyo wa chuo cha ulinzi ameipongeza serikali ya mkoa wa Mara kwa usimamizi mzuri wa hospital na kuhakikisha malengo ya serikali yanafikiwa.

” Tumetembelea hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere hapa Musoma na kuona na kupewa taarifa ya shughuli na huduma zinazotolewa hapa.

” Tunaipongeza serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya ukamilishwaji wa hospital hii ili wananchi waendelee kupata ulinzi wa afya zao.

” Uongozi wa hospital chini ya Dk.Dyagura na watumishi wote tunawapongeza kwa kazi nzuri mnazozifanya kwa kuwahudumia wananchi”,amesema.

Aidha ameongeza kuwa hospital hiyo haipo kwaajili ya rufaa kwa wananchi wa mkoa wa Mara pekee pia inapokea watu kutoka nchi jirani kwaajili ya utalii wa kimatibabu.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dk.Osmund Dyagura amesema changamoto zilizotolewa na viongozi walio watembelea wanakwenda kuzifanyia kazi ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!