Home Kitaifa HIVI NDIVYO KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDLEO INAVYOENDELEA JIMBO LA...

HIVI NDIVYO KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDLEO INAVYOENDELEA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

JIMBO la Musoma vijijini ni moja ya majimbo ambayo yanapiga kasi kubwa kwenye masuala ya miradi ya maendeleo kwa ushirikiano wa mbunge wa jimbo na wananchi na fedha nyingi zinazotolewa na serikali.

Kwa kuthibitisha hilo septemba 27 na 29 mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo amepanga kuendesha harambee za ujenzi wa shule mpya 2 ndani ya jimbo hilo.

Hii yote ni kulifanya jimbo hilo kuendelea kufanya vizuri kwenye sekta ya elimu na kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea umbali mrefu.

Tuanze na sekta ya miundombinu tukianzia barabara za Musoma vijijini tukianzia na ya
-Makojo-Busekera ambapo Tanroads wako kwenye utaratibu wa manunuzi kwa ajili ya uwekaji lami kwenye barabara hii ambayo serikali imeamua kulijenga kwa awamu mbili.

Tayari mbunge wa jimbo amesema kwamba ujenzi unatafutiwa mkandarasi uwe wa kuendeleza ujenzi wa Lot 2 (Kusenyi-Makojo-Busekera) ambapo kilomita 5 za lami zilijengwa kwa miaka minne 4

Utengenezaji wa barabara ya Musoma-Mugango-Makojo-Busekera Tanroads mkoa wameanza matengenezo ya uboreshaji wa barabara hili kwa kipande cha Musoma-Mugango

Tukiachana na sekta ya miundombinu ya barabara upande wa kilimo cha umwagiliaj mambo yanakwenda kwa kasi.

Bonde la Bugwema
*”Consultant” ameanza kufanya “feasibility study” (tarehe 17.9.2023 – 16.10.2023).na mbunge ametoa taarifa kwamba atawatembelea wakiwa kazini Bugwema.

Mazao makuu yatakayolimwa kwa umwagiliaji ni mahindi, mpunga, alizeti, dengu, pamba na mboga mboga

Bonde la Suguti.
*”Consultant” atafanya “feasibility study” baada ya kukamilisha kazi kwenye Bonde la Bugwema

Sekta ya elimu ya sekondari maabara
zinaendelea na ujenzi wa vyumba 3 (Physics, Chemistry & Biology) kwa kila sekondari.huku wananchi wakichangia ujenzi huu na kuishukuru kila mara serikali inapouunga mkono kwa michango yake mikubwa

Halmashauri ya Musoma DC inaendelee kukumbushwa kuchangia ujenzi wa maabara 3 kwenye kila sekondari ya Kata kwa sasa xupo 25 na zunajengwaa mpya 5 sekondari za binafsi ni 2

Shule za ” High School”zinaendelea kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu muhimu inayotakiwa kwenye uanzishwaji wa science high schools.

Kinachohitajika kwa uanzishwaji wa “science high school” ni: maji ya bomba, maabara 3, bweni, na bwalo la chakula ambavyo vinaendelea kujengwa.

Lengo la jimbo ni mwakani 2024 liwe na angalau HIGH SCHOOLS 2-3 za masomo ya sayansi na Ile ya Kasoma ni ya masomo ya “arts.”

Elimu ya msingi miradi ya Boost shule za msingi tisa (9) zimepewa jumla ya shilingi bilioni 1.35 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule hizo.

Wananchi, mbunge wa jimbo na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya wamendelee kufuatilia mradi huu kwa ukaribu sana.

Shule za msingi zilizopewa fedha ni Bugoji, Buira, Bulinga B, Kanyega, Kataryo B, Kigera B, Mabuimerafuru B, Masinono na Nyambono B

Sekta ya maji ya bomba kutoka Muwasa hupelekwa kwenye Kata za Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu

Muwasa inaendelea kukusanya baadhi ya vifaa hitajika kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha.

Vilevile Muwasa imewasilisha serikalini bajeti ya kutekeleza mradi huu

Muwasa imeshaanza kusambaza maji ya bomba kwa baadhi ya maeneo ya kata hizi

Kijiji cha Nyasaungu cha Kata ya Ifulifu kimeanza kupata maji ya bomba kutoka kwenye bomba la zamani la Mugango-Kiabakari-Butiama

Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
Ajenzi umekamilika kwa asilimia 92 (92%) na ifikapo desemba 2023 kazi zote muhimu zitakuwa zimekamilishwa

Miundombinu ya usambazaji maji ndani ya Kata ya Tegeruka.

Maji ya bomba kwenye Kata hii yatatoka kwenye bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama mabomba yametandazwa ndani ya vijiji vyote vitatu vya Kata hii ambavyo ni Kataryo, Mayani na Tegeruka

*Tenki la ujazo wa lita 135,000 tayari linakamilishwa ujenzi kijijini Mayani

Miundombinu ya usambazaji maji ndani ya Kara ya Mugango
itapata maji ya bomba kutoka kwenye bomba la Mugango- Kiabakari-Butiama

Mabomba yamesambazwa kwenye vijiji vyote vitatu vya Kata hii ambavyo ni Kwibara, Kurwaki na Nyang’oma.

Tenki la ujazo wa lita 500,000
limejengwa kwenye mlima Kong’u kijijini Nyang’oma

Miundombinu ya usambazaji maji kwenye Kata ya Busambara na Kiriba maji ya bomba ya Kata hizi mbili yatatoka kwenye Tenki la lita 500,000 liliojengwa mlimani Kong’u. Maji yake yatatoka kwenye bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama

Kwa upande wa Ruwasa imepata vibali vyote hitajika kutoka serikalini na ndani ya miezi miwili miundombinu ya usambazaji maji ya bomba ndani ya Kata hizi itaanza kujengwa.

Kata ya Bwasi Vijiji vyote vitatu vya Kata hii yaani Bwasi, Bugunda na Kome vinatandaziwa mabomba ya maji

Ujenzi wa tenki la ujazo wa lita 150,000 tayari limekamilishwa Kijijini Bwasi

Miundombinu ya usambazaji maji ya bomba kwenye vijiji vya Chumwi na Mabuimerafur ujenzi wa tenki la ujazo wa luta 300,OOO umekamilika kijijini Mabuimerafuru huku mabomba yakielendelea kutandazwa

Maji kutoka kwenye tenki hili yatasambazwa kwenye vijiji vya Masinono na Bugwema (Kata jirani ya Bugwema)

Maji ya kisima cha Rusoli sekondar yanaendelea kusaidia na shukrani zinatolewa kwa baadhi ya wazaliwa wa Rusoli kwa ufadhili wa uchimbaji wa kisima hiki.

Ruwasa imekamilisha ujenzi wa tenki la lita 75,000 kwa ajili ya usambazaji wa maji kijijini hapo.

Bado tunaendelea kuliangalia jimbo la Musoma vijijini na tuangazie sekta ya afya.

Hospital ya Halmashauri yenye hadhi ya hospital ya Wilaya imeanza kutoa huduma za afya kwenye Kitongoji cha Kwikonero Kijiji cha Suguti.

Hospitali hii inavyo vifaa tiba vya kisasa ikiwemo Digital X-ray, Ultrasound, vifaa vya upasauji na mitambo ya kutengeneza Oxygen.

Kwa sasa jumla ya vituo vya afya sita (6) ambavyo ni: (i) Murangi, (ii) Makojo (mpya), (iii) Kiriba (mpya), (iv) Kisiwa cha Rukuba zahanati yake imepanuliwa), (v) Mugango (Zahanati yake imepanuliwa), na (vi) Bugwema (ilikuwa zahanati ya Masinono, imepanuliwa)

Jumla ya zahanati 42 zipo jimboni huku
zaahanati 24 zinatoa Hhuduma za afya vijijini na zahanati 14 zinaendelea kujengwa na baadhi karibu zitakamilishwa ujenzi,
zahanati 4 za binafsi zinatoa huduma za afya vijijini.

Tunaipongeza sana serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kasi hii ya kupeleka fedha nyingi za maendeleo jimbo la Musoma vijijini.

Tunampongeza pia mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo kwa ufatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali jimboni.

Na mbunge Muhongo anasema ataendelea kufuatilia miradi ya usambazaji umeme vijijini (REA NA TANESCO) huku akidsi miradi ya REA itaanza hivi karibuni

Ataendelea kufuatilia miradi ya ujenzi na uboreshaji wa barabara jimboni kupitia(TARURA NA TANROADS)

Atafatilia pia uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji maji ya bomba vijijini kwa kupitia (RUWASA & MUWASA)

Tunaendelea kukupongeza kwa dhati Profesa Sospeter Muhongo kwa kuwatumikia wananchi wa jimbo la Musoma vijijini na mwenye macho haambiwi tazama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!