Home Kitaifa HEKARI 807 ZA MASHAMBA ZATEKETEZWA MKOANI MARA

HEKARI 807 ZA MASHAMBA ZATEKETEZWA MKOANI MARA

Ashrack Miraji

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa, askari mgambo pamoja na vyombo vingine vya dola, imefanya operesheni maalum Mkoani Mara hususani katika Kanda maalum ya Tarime Rorya kwenye Bonde la Mto Mara.

Operesheni hii, iliyofanyika kuanzia October 02 hadi 08, imefanikisha uteketezaji wa jumla ya hekari 807 za mashamba ya bangi, ukamataji wa gunia 507 za bangi kavu iliyo tayari kusafirishwa, gunia 50 za mbegu za bangi pamoja na kuteketeza viwanda viwili vidogo vilivyokuwa vikitumika kuchakata na kufunga bangi kabla ya kusafirishwa ambapo Watuhumiwa 11 wanashikiliwa kuhusika na dawa hizo.

Akiongea katika tukio hilo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, wakazi wa eneo hilo wamelifanya Bonde la Mto Mara kama eneo maalum kwa ajili ya kilimo cha bangi na kujimilikisha kwa kutoruhusu Mtu yeyote asiye mkazi kuingia kwenye Bonde kama sehemu ya kuficha uharifu wao na wametishia kumdhuru yoyote atakayeingia ndani ya Bonde hilo bila ridhaa yao “Wamediriki hadi kufunga ofisi ya kijiji wakimtuhumu Mtenda wa kijiji cha Nkerege kutounga mkono kilimo cha bangi”

‘‘Sisi kama Mamlaka tutafanya operesheni endelevu katika maeneo haya kuhakikisha kilimo cha bangi kinaisha, Bonde hili lina rutuba nyingi na linakubali mazao ya aina zote, hivyo tumekubaliandani RC wa Mara kuwa na mikakati ya kusimamia Bonde ili kumaliza kilimo cha bangi na kutafutwa kwa shughuli nyingine ambayo itakuwa rafiki’

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!