Home Kitaifa HARAMBEE YA MBUNGE MUHONGO SIKU YA MAPINDUZI ” DAY” ILIVYO FAFANIKISHA UPAUAJI...

HARAMBEE YA MBUNGE MUHONGO SIKU YA MAPINDUZI ” DAY” ILIVYO FAFANIKISHA UPAUAJI WA MADARASA YA SHULE SHIKIZI KIUNDA YA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

JANUARI 12 ilikuwa ni maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ambapo ilishuhudiwa uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo huko visiwani Zanzibar.

Jimbo la Musoma vijijini lililopo mkoa wa Mara kama sehemu ya Muungano liliungana na Wazanzibar kusherehekea tukio hilo lililofanyika miaka 60 iliyopita.

Mbunge mpenda maendeleo ya kijamii Profesa Sospeter Muhongo katika kuhadhimisha siku hiyo ya kumbukumbu ya Mapunduzi aliongoza harambee ya ujenzi wa shule shikizi ya Kiunda katika Kata ya Nyakatende.

Harambee hoyo ililenga kukamilisha kazi ya upauaji wa boma la shule shikizi Kiunda ya Kijiji cha Kamguruki Kata ya Nyakatende.

Boma hilo ni la vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu ambapo boma limejengwa kwa michango ya wananchi wa Kitongoji cha Kiunda, diwani wa Kata na mbunge wa jimbo hilo.

Jimbo la Musoma vijijini lenye Kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374 ina shule za msingi za serikali 111 na 4 shule binafsi huku shule 12 shikizi zinazopanuliwa

Kwenye harambee ya shule shikizi Kiunda
gharama zote za upauaji zilizo hitajika ni shilingi milioni 4,268,000

Fedha zilizopatikana kwenye harambee ni shilingi miliomi 1,285,000 wachangiaji wakiwa wakazi wa Kijiji cha Kamguruki ,wakazi kutoka Vijiji jirani
“DEO” Hamisi Shemahonge,viongozi wa Chama cha Mapinduxi Wilaya na jumuiya zake ambao ni Jackson Nyakia, William Magero, Bwire Mkuku na Sophia Maregesi

Aidha wapo wadau waliochangia mabati kwenye harambee hiyo ambao ni Pascal Maganga mabati 24,diwani Kisha Marere mabati 36 na mbunge Prof. Muhongo mabati 72

Tayari ratiba ya upauaji imepangwa kufanyika februari 23 mwaka huu huku mafundi wakitakiwa kuanza kuweka mbao za paa.

Kaimu Mtendaji wa Kijiji (VEO) Magreth Malima amepewa pongezi nyingi kwa usimamizi mzuri wa shughuli za maendeleo ndani ya Kijiji cha Kamguruki

Bado michango inarndelea kukaribishwa kutoks kwa
Wana-Kitongoji cha Kiunda na Kata ya Nyakatende kwa ujumla wanaendelea kuomba michango kutoka vyanzo mbalimbali ili kujenga na kupanua shule shikizi Kiunda iwe Shule ya msingi kamili inayojitegemea.

Kwa wachangiaji michango ielekezwe kwenye akaunti ya Kijiji cha Kamguruki.
iliyopo benki ya NMB kwa
akaunti namba 30302300679 jina la akaunti Kijiji cha Kamguruki

Wakazi wa Kitongoji cha Kiunda na Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Harambee iliyofanyika kwenye eneo la ujenzi wa Shule Shikizi Kiunda ya Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende, Musoma Vijijini.

Katika kuinua kiwango cha elimu hususani jimbo la Musoma vijijini hakuna budi kumshukuru mbunge wa jimbo hilo profesa Sospeter Muhongo kwa jitihada zake za kuongoza harambee mbalimbali na wadau wote wanao muunga mkono.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!