Home Kitaifa HALMASHAURI YA MUSOMA VIJIJINI YAJIPANGA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

HALMASHAURI YA MUSOMA VIJIJINI YAJIPANGA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Na Shomari Binda-Musoma

HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma vijijini imejipanga kutatua na kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo inayochangia kurudisha nyuma maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Msongela Palela kwenye kliniki ya kusikiliza migogoro ya ardhi inayoendelea Kijiji cha Bukima.

Amesema ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara lengo lake la kuanzisha kliniki hiyo ni kuwafuata wananchi na kuwasikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi.

Msongela amesema migogoro ya ardhi imekuwa ikichangia kurudisha nyuma marndeleo kutokana na kutumia muda mwingi kuifatilia.

Amesema kufika kwenye kliniki hiyo itakayo wahudumia wananchi kwa Siku 2 katika eneo la Bukima itakuwa ni fursa nzuri ya kuwasikiliza wananchi.

Mkurugenzi huyo amesema wananchi wasisubili viongozi wa kitaifa wanapofika na kutoa kero zao bali watumie fursa hiyo kuimaliza.

“Leo tumewafata wananchi kwenye maeneo yenu kuwasikiliza mmekuja wachache baadae wakija viongozi wa kitaifa mnajitokeza na mabango”

“Tutakuwa hapa kwa siku 2 kabla ya kwenda Busekera naomba tupeane taarifa na kukitokeza kwa wingi ili tuweze kusikiliza migogoro itakayojitokeza” amesema Msongela.

Kaimu Kamishina Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Mara Dickson Mwinuka amesema wamejianga kumaliza migogoro iliyopo ili shughuli nyingine za kiuchumi ziweze kuendelea.

Amesema wataalam wa idara ya ardhi halmashauri ya Musoma na ofisi ya Kamishina Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Mara ipo tayari kuyafikia maeneo ya migogoro na kuitatua.

Kwa upande wao wananchi wa Kijiji cha Bukima wsmeishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara kwa kuanzisha kliniki hiyo ya utatuzi wa migogoro ya ardhi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!