Home Kitaifa HAKIELIMU YATOA MATOKEO YA UTAFITI MCHANGO WA ELIMU YA URAIA SHULE ZA...

HAKIELIMU YATOA MATOKEO YA UTAFITI MCHANGO WA ELIMU YA URAIA SHULE ZA SEKONDARI

Na Magreth Mbinga

Taasisi ya hakielimu imebaini kuwepo kwa changamoto kubwa katika mtaala wa somo la uraia katika shule za sekondari ambao kwa kiwango kikubwa haumpi mafunzo stahiki mwanafunzi yatakayo mfanya aelewe vyema na kushiriki shughuli za kidemokrasi.

Hayo yamezungumzwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya hakielimu Godfrey Boniventura wakati wa uzinduzi wa utafiti huo Septemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam ambapo amesema utafiti huo umejumuisha Wilaya kumi ambazo zimwtosheleza kufanya utafiti huo.

“Kwa mujibu was utafiti huu vijana wanatarajia kuwa shule ndio chanzo kikuu cha kujifunza na kujengewa uzoefu katika michakato ya kidemokrasia ukilinganisha na redio ,televisheni,magazeti,mitandao ya kijamii na kujisomea” amesema Boniventura.

Pia Boniventura amesema takribani asilimia 40 ya wanafunzi hawajapata fursa ya kuwa viongozi baadhi ya walimu wanachagua wanafunzi ambao wana wahitaji wawe viongozi hiyo ni changamoto ambayo tumeiona .

Aidha Kamishna wa Elimu Liabwene Mtahabwa amesema utafiti hio umekuja wakati muhafaka Mh Rais Samoa Suluhu Hassan amesema yafanywe mapitio ya mitaala ya Elimu ya Tanzania ili kuwajengea wanafunzi ujuzi WA kuwafanya waweze kuona fursa katika mazingira yao na kuweza kusimama kwa miguu yao wakaweza kujitegemea.

“Nimeona mapendekezo yaliyomo ndani ni mazuri sana na yamekuja wakati muhafaka tayali mchakato wa kupitia unaendelea kwahiyo utafiti huu utapelekwa kwenye kamati ya Kitaifa amvayo imeundwa inayosimamia zoezi la mapitio ya mitaala na sasa tupo hatua nzuri ili tutalibeba na tutaliingiza katika mitaala yetu” amesema Mtahabwa.

Sanjari na hayo Mtahabwa amesema demokrasia nivyema ijengwe juu ya msingi wa uzalendo ule wa kumaanisha Nchi ndipo itaweza kuimarika na kuleta yale ambayo yataimarisha Taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!