Home Kitaifa HAKIELIMU YATOA MAPENDEKEZO KATIKA BAJETI YA SERIKALI KWENYE SEKTA YA ELIMU

HAKIELIMU YATOA MAPENDEKEZO KATIKA BAJETI YA SERIKALI KWENYE SEKTA YA ELIMU

Taasisi ya hakielimu imesema ni wakati sahihi kama taifa kutumia lugha ya kiswahili kama lugha ya kufundishia inaweza kuandaa watoto kutumia kiswahili.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji Hakielimu John Kalage wakati akichambua mapendekezo ya bajeti ya Serikali nakushauri kwamba kingereza kifundishwe kama lugha ya kigeni ili watoto wajifunze kwaajili ya kushindana kikanda na kimataifa.

“Ikumbukwe matumizi ya lugha ya kiswahili ni matakwa ya Kisera, tamko no. 3.2.19 la sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 ambalolinasema, Lugha ya Taifa ya kiswahili itatumika kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote za elimu na mafunzo na Serikali itaweka utaratibu wa kuwezesha matumizi ya lugha hii kuwa na mafunzo yenye tija Kitaifa na Kimataifa “Arsenal Kalage.

Pia Kalage amesema Serikali ihakikishe inaongeza bajeti kwenye sekta ya elimu wanafunzi wanapoongezeka kuweza kusaidia utoaji wa elimu bora

“Ni rai yetu kuwa bajeti ya utoaji elimu iongezwe ili kufidia gharama hizi zinazoongezeka kwa upande wa Serikali, utoaji wa elimu bila malipo unafanyika kwa njia ya kupeleka ruzuku shuleni kwa viwango vya sh 10,000 kwa mwanafunzi wa elimu ya msingi kwa mwaka na sh 25,000 kwa mwanafunzi wa Sekondari kwa mwaka” amesema Kalage.

Aidha, ameendelea kusema kuwa kufutwa kwa ada ya kidato cha tano na sita ni moja kati ya pendekezo muhimu sana ambalo Hakielimu wanaunga mkono nakusema kuwa uamuzi huo kama utatekelezwa unatarajia kuwanufaisha takribani wanafunzi 95,000 wa kidato cha tano na zaidi ya 60,000 wa kidato cha sita wanaojiunga na kufanya masomo yao katika shule za umma ambao wengi wao hutokea familia zenye kipato cha chino.

Vilevile Kalage ametoa mapendekezo yao kama Hakielimu kuwa Serikali iangalie mahitaji halisi ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita na ijiepushe kupeleka ruzuku katika kiwango na utaratibu unaotumika kwa madarasa ya chini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!