Home Biashara HAIPPA PLC TANZANIA YATOA ELIMU YA BIASHARA

HAIPPA PLC TANZANIA YATOA ELIMU YA BIASHARA

Na Shomari Binda-Musoma

KAMPUNI ya umma ya iliyojikita kufanikisha biashara,uwekezaji na masoko ya Haippa PLC Tanzania imekusudia kuendelea kutoa elimu kwa watanzania waielewe na kuitumia kuwainua kiuchumi.

Hayo yamesemwa na meneja uwekezaji wa kampuni hiyo Wiseman Joshoa alipozugumza na Mzawa Blog kwenye shughuli za wiki ya Sheria inayoendelea uwanja wa shule ya msingi Mukendo.

Amesema kampuni hiyo ni suluhisho la kuwaondoa watanzania kwenye umasikini iwapo wataitumia katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Meneja huyo wa uwekezaji amesema ushiriki wao kwenye wiki hii ya Sheria ni kuendelea kuwapa elimu wananchi namna wanavyoweza kunufaika pale watakapo jisajili na kuwa familia ya Haippa.

Amesema unapo jisajili na Haippa unapata fursa ya kupata elimu uwekezaji, masoko na ubunifu na jinsi ya kujipatia fedha na kukuza uchumi.

Joshua amesema tangu kuanzishwa kwa Haippa oktoba 22 mwaka 2022 wamesha sajili watu wasiopungua 400 na kuwa na mtaji wa milioni 200.

Kujisajili ni rahisi hata kupitia simu ya mkononi kwa kupiga 14946*23# na kuendelea kupata maelezo na kufikia mwisho wa usajili.

Unapokamilisha unakuwa mwana familia na kukutana na wabobezi mbalimbali wa masuala ya uchumi na kukupa elimu itakayokuwezesha kunufaika kiuchumi”,amesema Joshua.

Ameongeza kuwa lengo la Haippa ni kuchangia hadhima ya serikali kuwafanya wananchi kujiajili na kupunguza makali ya uchumi kwenye maisha yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!