Home Kitaifa HABARI NJEMA KWA WAPENZI WA SOKA : HII HAPA FURSA YA KUSHUHUDIA...

HABARI NJEMA KWA WAPENZI WA SOKA : HII HAPA FURSA YA KUSHUHUDIA EURO CUP BURE ” ZIGO LA EURO CUP NA HISENSE “


William Mshery Mkazi wa Dar es Salaam ( Kushoto ) ambaye ni mshindi wa tiketi ( Wiki ya Nne ) Kampeni ya ZIGO la EURO CUP na Hisense, safari iliyolipiwa kila kitu  kwenda kutazama mechi za Kombe la Euro moja kwa moja nchini Ujerumani kuanzia hatua ya 16 bora, akikabidhiwa Mfano wa Tiketi tukio lililofanyika mapema leo hii June , 21 , 2024 Makao makuu ya Tigo Jijini Dar Es Salaam , Bwn. Ashery ameibuka mshindi baada ya kubashiri Mechi na PariMatch kupitia Tigo Pesa Super App, katikati ni Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta na Mwakilishi wa Hisense Jacob Kam , Kulia ni Balozi wa PARIMATCH Mchekeshaji Mama Chanja.

Na Adery Masta.

William Mshery Mkazi wa Dar Es Salaam, ni Mteja wa Tigo wa nne kujishindia Safari iliyolipiwa kila kitu ya kwenda kutazama Mechi za Kombe la EURO 2024 , ambapo timu 24 zinatarajiwa kuchuana katika miji 10 mwenyeji Nchini Ujerumani . 

William  ameshinda kupitia Kampeni ya ZIGO LA EURO CUP NA Hisense , iliyozinduliwa wiki kadhaa Zilizopita ambapo Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO, kwa kushirikiana na Parimatch na Hisense waliileta kusambaza Tabasamu kwa Wateja wao , Ikumbukwe Willliam ni Mshindi wa Wiki ya nne akitanguliwa na Aida Juma,  Ramadhan Mrutu Mshindi wa Wiki ya Kwanza  na Emmanuel Mlonjela Mshindi wa Wiki ya Pili , Ikumbukwe ndani ya Wiki Nne sasa Tigo , PariMatch na Hisense wameshatoa zawadi za Vifaa vya Hisense ( TV na Friji ) , Pesa Taslimu, na Tiketi za Kushuhudia EURO kwa Watanzania zaidi ya 24.

Ili kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia tiketi au zawadi ya fedha taslimu TZS 1,000,000, na Vifaa vya Hisense TV na Friji washiriki wanapaswa kujiandikisha na Parimatch, kuweka pesa zao kupitia Tigo Pesa kisha kuweka dau ( betting ) kwenye mechi yoyote ya mpira wa miguu na Parimatch. Kadiri dau zinavyowekwa, ndivyo nafasi zinavyoongezeka ya kushinda TZS 1,000,000 au tiketi ya safari na mechi yenye malipo kamili ya kwenda kutazama mechi za Kombe la Euro moja kwa moja nchini Ujerumani kuanzia hatua ya 16 bora.

Akizungumza Wakati wa Kugawa zawadi kwa Washindi , Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta amesema 

” Ndo kwanza ni droo ya NNE ya Kampeni yetu ya ZIGO LA EURO na Hisense , kama ambavyo inajulikana Kampeni hii tunatafuta Washindi wa Tiketi ya Kwenda kushuhudia Mechi za Euro ambalo Mechi tayari zimeanza rasmi , Washindi wa Vifaa vya Hisense ambavyo ni Friji na Tv ya Kisasa , na Washindi wa Pesa Taslimu ambapo hadi sasa Tumeshatoa zawadi kwa Watanzania zaidi ya 24

Zawadi bado zipo nyingi kwa maana Leo ndo Washindi wa Droo ya nne, bado Kuna Droo nyingine nyingi zinawasubiri , Tumia kwa wingi TIGO Pesa Super App , Bashiri na Parimatch kupia App ya Tigo Pesa ili kutengeneza mazingira ya kujishindia zawadi za Tv na Friji kutoka Hisense , Fedha Taslimu Hadi Milioni Moja na Zawadi kubwa ya kwenda kushuhudia Mechi za EURO CUP 2024 ” alimalizia Mary Ruta

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!