Home Biashara GST YAJIPANGA KUKAMILISHA TAFITI ZA MADINI CHUNYA

GST YAJIPANGA KUKAMILISHA TAFITI ZA MADINI CHUNYA

Kampuni ya Goldorox Tanza Ltd yaipongeza GST kwa kasi, weledi na ubora wa vifaa

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imejipanga kikamilifu kuhakikisha inakamilisha tafiti katika leseni za Mwakezaji Mohamed Altesbehji anaye miliki Kampuni ya Goldorox Tanza Ltd kutoka Dudai zilizopo katika Mkoa wa Kimadini Chunya.

Kauli hiyo ameitoa Mkurugenzi wa Huduma za Jiolojia kutoka GST Dkt. Ronald Massawe baada ya kutembelea eneo la leseni la Kampuni hiyo ambapo amesema Tanzania inahitaji wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi hivyo atahakikisha kazi ya tafiti katika maeneo hayo inakamilika kwa wakati na kwa weledi mkubwa.

Wakati akikagua maendeleo ya kazi hiyo, Dkt. Massawe amesema kuwa, kazi inaendelea vizuri kama ilivyopangwa na mteja wao atapatiwa ripoti yake kwa wakati ili imsaidie kufanya maamuzi sahihi kwenye utafiti wa kina ukiwemo uchorongaji.

Akielezea utekelezaji wa utafiti huo, Dkt. Massawe amesema GST imejipanga vizuri na kazi hiyo ya utafiti unaofanywa na timu tatu za wataalamu ambazo ni timu ya jiolojia, jiokemia na jiofizikia ambapo kila timu inaendelea na kazi yake kama ilivyojipangia.

Naye, mtaalamu wa GST aliyeambatana na timu hiyo wakati wa ukaguzi wa namna kazi inavyofanyika Mjiolojia Mwandamizi Charles Moye ameelezea namna utafiti ulivyofanyika na hatua iliyofikia sambamba na jiolojia inavyojipambanua kwenye eneo la utafiti.

Kwa upande wake, Mwekezaji Mohamad Altesbehji ambaye ni mwekezaji kutoka Dubai chini ya kampuni ya Goldorox Tanza Ltd amesema kwamba, amevutiwa na kasi na weledi uliooneshwa na wataalam wa GST wanaoendelea kufanya utafiti wa madini katika leseni zake zilizopo wilaya ya Chunya.

“Nimeridhishwa sana na utendaji kazi wa GST, wataalamu wameonesha uzoefu na weledi mkubwa sana na nimeona wanatumia vifaa vya kisasa, GST mpo vizuri,” amesema Altesbehji.

Aidha, mwekezaji huyo amesema kuwa kwa kasi ambayo wataalamu wa GST wameonesha katika kufanya utafiti huo, anaamini kazi hiyo itakamilishwa kwa wakati.

Pia, ameipongeza GST kwa namna ilivyoratibu utekelezaji wa kazi yake ambapo mpaka sasa tafiti katika leseni hizo zinakwenda kwa kasi na kwa uhakika mkubwa.

Katika ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya kazi hiyo Dr. Massawe amembatana na wataalamu mbalimbali akiwemo Meneja sehemu ya Jiolojia Maswi Solomon, Meneja Masoko na Mipango Priscus Benard na Mkaguzi Mkuu wa Ndani CPA Timoth Mbulla lengo engo kuu likiwa ni kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa kazi hiyo kwa mujibu wa viwango vya ubora vilivowekwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!