Home Kitaifa GRUMENT FUND YATOA MSAADA JESHI LA POLISI MKOA WA MARA KUKABILIANA NA...

GRUMENT FUND YATOA MSAADA JESHI LA POLISI MKOA WA MARA KUKABILIANA NA UHALIFU

Na Shomari Binda-Musoma

TAASISI ya Grument Fund inayoshughulika na masuala ya uhifadhi imesadia jeshi la polisi mkoa wa Mara usafiri wa bajaj maalum ya kubeba mbwa wa ulinzi na chakula kwaajili ya kuzuia uhalifu.

Msaada huo wenye jumla ya shilingi milioni 24 na laki 3 umekuja wakati jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali likiendelea kukabiliana na uhalifu na wahalifu ikiwemo kulinda nyara za taifa.

Akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo,meneja mtendaji wa Grument Fund, Matt Perry amesema mara kadhaa wamekuwa wakishirikiana na jeshi la polisi katika kukabiliana na uhalifu na huo ni muendelezo.

Amesema licha ya kusaidia usafiri huo kwa ajili ya safari fupi za kusafirisha mbwa wa ulinzi na chakula cha mbwa wameandaa mafunzo maalumu mwezi septemba mwaka huu kwa askari wa kikosi cha mbwa.

Matt amesema mafunzo hayo yatawasaidia askari wa jeshi la polisi kikosi cha mbwa mkoa wa Mara na itakuwa ni muendelezo wa kukabiliana na uhalifu.

“Mafunzo haya ya kutumia mbwa kutumia mbwa kuzuia uhalifu yatakuwa msaada mkubwa katika kuzuia uhalifu na huu ni ushirikiano mzuri” amesema Matt.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Camilius Wambura,mkuu wa vikosi maalum vya jeshi la polisi, Naibu Kamishina(DCP) Ferdinand Mtui, ameishukuru taasisi hiyo kwa msaada walioutoa.

Amesema kupambana na uhalifu na wahalifu sio kazi ya jeshi la polisi pekee bali ni jukumu la kila mmoja na kuwashukuru Grument Fund kwa kile walichokitoa.

Mtu amesema mbwa ni moja ya walinzi wazuri katika kuzuia uhalifu na wahalifu na kuwaomba wananchi kuwa na mwamko wa kufuga mbwa.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mara,Salim Morcase,amewashukuru Grument Fund na kudai msaada huo utasaidia kuimalisha masuala ya ulinzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!