Home Kitaifa GLOBAL LINK YANUFAIKA NA ZIARA ZA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSANI KWENDA...

GLOBAL LINK YANUFAIKA NA ZIARA ZA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSANI KWENDA NJE YA NCHI

Na Magrethy Katengu

Taasisi ya Global Education link (GEL)imesema kuwa imenifaika na Ziara za nje ya nchi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani serikali ya awamu ya sita kwa kufungua milango ya elimu jambo lililochochea muingiliano wa elimu baina ya Tanzania na mataifa mbalimbali duniani.

Ameyasema hayo Leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa taasisi hiyo,Abdulmalik Mollel wakati akizungumza na wadau mbalimbali ikiwemo wazazi na wanafunzi, wanaosoma Nje ya Nchi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja, hafla iliyofanyika katika ofisi kuu za taasisi hiyo Jijini Dar es salaam.

Mollel amesema ,serikali kufungua mipaka yake katika sekta ya elimu imeijengea Tanzania imani kubwa kwa wageni na Duniani kwa ujumla juu ya upatikanaji wa Elimu bora nchini kwani Taasisi hiyo imekuwa ikiwaunganisha wanafunzi kusoma nje ya nchi na wengine kuja kujiunga na vyuo vya Tanzani kusoma hivyo kwa ziara za Rais wameona fursa kubwa.

”Nikiri kuwa Ziara za Rais Daktari Samia nje ya nchi zimefungua wigo mpana wa Tanzania kufahamika na kutambulika na baadhi ya nchi kuleta wanafunzi Tanzania kupitia global link kusoma katika vyuo vikuu hapa nchini ikiwemo wanafunzi wa Sudani,China huku wanafunzi wa india wakija kufanya mafunzo kwa vitendo (field) Tanzania” amesema Mollel

Ameongeza kuwa global link kama taasisi imeona mchango mkubwa wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya ambayo imechangia global link kuwapeleka wanafunzi wa Kitanzania katika vyuo mbalimbali duniani hususani Nchini India kusomea kada mbalimbali za Afya katika ngazi ya Udaktari.

“Sisi kama Global Education link tutaendelea kushirikiana na serikali, wazazi na wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali ili kuendelea kuwa chachu ya mafanikio ya elimu ndani na nje ya Nchi”.

Akizungumzia wanafunzi waliokwama nchini Sudani kutokana na vita inayoendelea nchini humo amesema tayari wanafunzi hao wamedahiliwa katika vyuo mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi ambapo zaidi ya wanafunzi 1,800 wamedahiliwa.

Global Education link imefanikiwa kuwadahili wanafunzi wakigeni zaidi ya 420 kwenye vyuo mbalimbali hapa nchini ikiwemo India na china.

Naye Mzazi Anna Massawe ambaye ni miongoni mwa wazazi ambao watato wao wanasoma nje ya nchi kupitia global Education link ameshukuru namna watoto wake walipofikia na amesema kuwa, taasisi hiyo imkuwa mstari wa mbele ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya wanafunzi hao wanaosoma Nje ya Nchi na sio kumwachia jukumu hilo mzazi pekee.

Sambamba na hayo amemtakia Rais Dkt Samia safari njema anapoelekea Ziara yake nchini India Mungu amtangulie na amjalie afya njema na Baraka za Mungu andelee kufungua fursa nyingi zaidi na zaidi.

Pia amewasisitiza wazazi kutokuangalia gharama waangalie namna wanavyopata huduma bora ambayo hawawezi kuipatata popote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!