Home Kitaifa GEKUL AWATAKA MAHAKAMA KUSHIRIKIANA NA UTU KWANZA KUWAPA MSAADA YA KISHERIA WAFUNGWA...

GEKUL AWATAKA MAHAKAMA KUSHIRIKIANA NA UTU KWANZA KUWAPA MSAADA YA KISHERIA WAFUNGWA NA MAHABUSU WASIO NA UWEZO

NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul ameagiza Mahakama na jeshi la Polisi kuona ni namna gani wanaweza kushirikiana na shirika lisilo la kisheria la Utu Kwanza katika kusaidia upatikananji wa msaada wa kisheria kwa wafungwa na mahabusu wasio na uwezo ili wapate haki.

Gekul aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akifungua dawati la Msaada wa kisheria lililoanzishwa na Shirika lisilo la kiserikali Ia Utu kwamza ambalo limejipanga kutoa huduma ya Msaada wa kisheria katika mahakama nchini ingawa kwa kuanzia wanaanza katika Wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam.

Vilevile alisema Mashirika hayo yanatakiwa kushirikiana na Serikali katika kuboresha maisha ya watu wote huku wakizingatia kipaumbele cha utu kwenye haki jinai na wote wana wajibu wa kuwatumikia Watanzania katika kudumisha amani na mshikamano.

Aidha alisema wadau wa sheria na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na kutoa msaada wa kisheria yanatakiwa kutumia rasilimali zake vizuri kuwafikia walengwa.

Naibu Waziri huyo alisema Wizara inatambua jitihada za Shirika la Utu kwamlnza katika kuboresha maisha na utu kwa wafungwa na mahabusu kwa kipindi cha miaka sita tangu kuanzishwa kwake hususani kwa mkoa wa Dar es Salam.

“Kupitia muhimili wa Mahakama na sisi tutalisukuma ili ione namna ya kuridhia kuanza kwa dawati hilo bila kuathiri shughuli za kimahakama, ni matarajio yetu shirika litaendelwa kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria” alisema.

Mkurugenzi wa Utu kwanza Wakili Shehzada Walli alisema lengo la kuanzisha shirika hilo ni kusaidia wafungwa na kwamba dawati la kutoa msaada wa kisheria litasaidia watu ambao wanafikishwa polisi hawana msaada wa kuweza kuwajulisha ndugu na yeyote kuhusiana na kile kinachoendelea.

“Sisi hapa tumeona tukiweka dawati letu Mahakama ya Mwanzo na Wilaya litaweza kuwasaidia hawa watu litaweza kuwasaidia, kwanza kuwauliza hali zao na kuwauliza kama wamewapigia ndugu au marafiki ambao wanaweza wakawasaidia”

Lakini pia wataweza kutoa mafunzo ya nini kinafanyijka anapoenda mbele ya Hakimu anapataje dhamana kwa kutumia kitambulisho cha Taifa NIDA au barua kutoka Serikali ya Mtaa mtumishi wa shirika hilo atasaidia kufanikisha ili mhitaji aweze kupata dhamana na msaada mwingine.

Kwa kufanya hivyo itapunguza udadi ya watu ambao wangeenda kukaa gerezani ambao wangeweza kupata msaada huo wa kwanza na wameanza na Mahakama ya Kinondoni Mahakama ya Mwanzo na Wilaya na tayari wameomba ruhusa ya kuweka dawati hilo.

Alibainisha kwamba upo mradi wa nyumba salama kwa watoto ambao wazazi wao wapo gerezani na wale ambao wanazaliwa gerezani na wakirudi mtaani hawana wakuwatunza.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mansoor Altaf Hiran alisema kuwepo kwa dawati hilo ni jambo la muhimu kwani itasaidia wananchi kupata hali zao na kwamba kila mtu akipata haki yake amani itakuwepo.

Inpekta Msafiri Kundi kutoka gereza la Keko alisema dawati hilo likianza litakuwa na msaada kwa wafungwa na mahabusu kwani wapo baadhi yao hawana uwezo wa kupata Mawakili.

Katika ufunguzi huo wadau mbali mbali walijitokeza kukimbia mbio za km 60 kutoka Bagamoyo hadi na wengine Km 25 kwa mbio za baiskeli na km kumi na nyingine km tano.
++++++++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!