Home Kitaifa GAVU: RAIS DK. SAMIA, DK. MWINYI WATAPEPERUSHA BENDERA YA CCM KATIKA UCHAGUZI...

GAVU: RAIS DK. SAMIA, DK. MWINYI WATAPEPERUSHA BENDERA YA CCM KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025.

*Asema wamefanya kazi kubwa, nzuri kutekeleza Ilani ya Uchaguzi 2020-2025

Kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinzuri (CCM), Katibu wa NEC, Idara ya Oganaizesheni ya Chama, Issa Haji Ussi ‘Gavu,’ amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ndiyo pekee watakaopeperusha bendera katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza leo Machi 26, 2024 alipomwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, kufungua mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar, Cavu amesema Rais Dk. Samia na Rais Dk. Mwinyi wamefanya kazi kubwa na nzuri.

Gavu akizungumza katika mafunzo hayo, yaliyotanguliwa na kongamano la kumshukuru Rais Dk. Samia kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 katika miaka mitatu ya uongozi wake lililoandaliwa na UWT.

“Watu wawili hao, viongozi wawili hao, ndiyo turufu na tegemeo la Chama Cha Mapinduzi hivi sasa. Hatuna mgombea mwingine atakayesimama kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ni Dk. Samia Suluhu Hassan.

Hakuna mgombea mwingine atakayesimama kwa nafasi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa tiketi ya CCM ni Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Katika kongamano hilo, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda alimkabidhi mgeni rasmi hati ya shukrani ya Rais Dk. Samia kumpongeza na kumshukuru kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa kishindo na sh. milioni mbili za kuchukulia fomu ya kuwania kiti hicho wakati utakapowadia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!