Home Kitaifa FEMATA yachanga zaidi ya milioni 768 kuanzisha benki yake

FEMATA yachanga zaidi ya milioni 768 kuanzisha benki yake

Wajumbe wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji madini nchini Tanzania (FEMATA) wamekubaliana kwa kauli moja kuanzisha benki ya wachimbaji madini ambapo zaidi sh milioni 768 zilichangwa kwenye maonesho ya wachimbaji wadogo Jijini Mwanza.

Fedha hizo zilipatikana kutokana na kuwepo kwa changamoto kubwa kwa wachimbaji madini kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha kwa kutokuwa na dhamana kuwawezesha kununua vyombo vya kisasa kwenye uchimbaji madini.

Naibu Waziri wa madini Dkt. Steven Kiruswa pamoja na mambo mengine amepongeza hatua ya kuanzishwa kwa benki hivyo aliagiza kuundwa kikosi kazi kuhakikisha wanasimamia uanzishwaji wake na kwamba serikali itawaunga mkono.

Alisema siku zote umoja ni nguvu hivyo wakishirikiana kwa pamoja watafanikisha lengo hilo walilonalo hivyo hatua hiyo italeta mabadiliko chanya kwenye sekta ya madini hapa nchini.

Baada ya makubaliano hayo Rais wa FEMATA, John Bina alipongeza juhudi hizo zilizofikiwa za kuanzisha mchakato wa benki ya wachimbaji wadogo.

Alisema hatua hiyo itawezesha wachimbaji hao kupata mikopo yenye masharti nafuu baada ya malalamiko ya muda mrefu ya kukosa sifa za kukopeshwa na mabenki nchini.

Mkurugenzi Mgodi wa Busolwa Baraka Ezekiel alisema waanze kwa vitendo ambapo alichanga milioni 200 taslimu kuondoa sintofahamu ya kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha nchini kwani inakwaza ukuaji wa wachimbaji wadogo hivyo kuendelea kutumia teknolojia ya zamani.

Alisema mafanikio yoyote yanafanywa kwa umoja baada ya kuunganisha nguvu pamoja na kudhamiria kufikia malengo yaliyokusudiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!