Waigizaji na Wasanii mbalimbali mkoaniMwanza, wamesema wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya sita kwenye ukusanyaji wa tozo na wao wako tayari kulipa tozo hizo kwa kuwa wanaridhishwa na jinsi zinavyotumika kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo mkoani humo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walipotembelea miradi maendeleo iiliyopo Mwanza, ikiwemo mradi mkubwa wa Uzalishaji maji uliopo chini ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mwanza (MWAWASA), na Mradi mkubwa wa Stendi ya Mabasi, Wasanii hao wameipongeza Serikali kwa Utekelezaji wa miradi hiyo kupitia tozo za wananchi.
“Mnaona huu mradi mkubwa wa Maji ambao utazalisha Lita za Maji Milioni 40, mimi kama Mtanzania niliyekamilika nimekubali kulipa TOZO” – Amesema Privatus Rwegoshora (Sharobaro wa Kihaya).
Kwa upande wake Msanii Evodia Julius maarufu kama Kasumali, amewasihi makundi mbalimbali ya wananchi hasa Wanawake kuunga mkono hatua ya ulipaji wa tozo za Serikali.
“Mimi kama Mama nawaambia wakina Mama wenzangu waliopo kwenyw vikundi na kwenye maeneo mengine tumuunge mkono mwanamke mwenzetu kwa kulipa tozo si mnaona maendeleo anayotuletea” Amesema Evodia Julius (Kasumali)