Home Kitaifa FDH YAIANGUKIA SERIKALI WENYE ULEMAVU KUKUOMBA MIKOPO YA HALMSHAURI KWENYE MITANDAO NI...

FDH YAIANGUKIA SERIKALI WENYE ULEMAVU KUKUOMBA MIKOPO YA HALMSHAURI KWENYE MITANDAO NI KIKWAZO.

Serikali imeombwa kuangalia namna ya kuwajengea uwezo wa jinsi kutumia mifumo ya mitandao watu wenye ulemavu ili na wao waweze kunufaika na fursa ya mkopo ya Halmashauri inayotarajia kuanza kutolewa nchini kote mwezi huu kupitia mfumo wa mitandao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Taasisi ya Foundation for Disabilities FDH Michael Salali wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma kuhusu harakati za taasisi hiyo kushiriki katika kudhibiti vitendo vya ukatili kwa wenye ulemavu nchini kupitia Mradi waliowezeshwa na taasisi ya Women Fund Tanzania Trust 

Amesema Kuna mapindizi makubwa ya matumizi ya mitandao ambayo ina faida na changamoto zake hasa ikizingatiwa kuwa kundi la wenye ulemavu lipo nyuma kwenye matumizi ya kiteknolojia na mitandao kutokana na sababu mbalimbali za kiulemavu.

“Mfano mweye ulemavu wa ukiziwi yeye hawezi kuendana na teknolojia inamuacha pembeni kwasababu taarifa zinachelewa kumfikia kwakuwa yeye anatumia lugha ya alama au ndugu zetu wasioona wanapotaka kuingia kwenye hiyo mifumo wanakutana na vikwazo vya kutokana na changamoto zao za kiulemavu” alisema.

“Lakini pia hii mifumo ya mitandao hutumika kutengeneza ukatili kwa wenye ulemavu tunashuhudia Kuna baadhi ya watu wameahapata kufanyiwa vitendo vya ukatili kupitia mitandao”

Alisema serikali inatarajia kuanza kutoa mikopo ya asilimia kumi ya Halmashauri jambo ambalo walikuwa wakilisubiri kwa muda mrefu lakini limekuja na kikwazo hicho ambacho kinaweza kuwakwamisha wenye ulemavu wasinufaike na mikopo hiyo.

“Lakini Sasa Kuna mfumo umetengenezwa ambao tunaweza kuomba mikopo mtandaoni kweli hapo kuna changamoto hivyo tunataka tuwajengee uwezo ili tuone namna ya kuweza kutumia ule mfumo waweze kukopa”

“Sasa kukiwa na mikopo na wasipoweza kutumia mfumo sisi tunatafsi tena huo ni ukatili hivyo tunataka kuona wanajengewa uwezo ili wenye ulemavu watumie ule mfumo wakope tusije kupata malalamiko kwamba sisi hatujapata au wamepata wachache” alisema.

Salali alisema Kuna kundi kama wenye ulemavu wa wasioona ambalo iwapo Halmashauri na serikali kwa ujumla lisipowekea mkakati maalumu kundi Hilo halitanufaika na mikopo hiyo ya Halmashauri kwani ni ngumu kwao kutumia mifumo ya mitandao kuomba mikopo hiyo.

Alisema taasisi hiyo katika kushughulikia tatizo hilo limeandaa mpango wa kukutana na viongozi wa Halmashauri nchini ili waone chakufanya ili kusaidia kundi Hilo na makundi mengine ya wenye ulemavu kuhakikisha yanawekewa mpango stahiki utakaosaidia wanufaike na mikopo hiyo ikiwa ni pamoja na kupitia mifumo ya kimtandao iliyowekwa.

“Tuwajengee uwezo hao wenye ulemavu ili waweze kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo kwa walemavu”

Alisema pia shirika hilo kwa kushirikiana na Wadau wake wakiwemo Women Fund wajipanga kuwajengea uwezo wa matumizi Bora ya mikopo hiyo kwa kundi hilo la wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kutumia mikopo hiyo kupata tija ili waondokane na umasikini.

“Tutawajengea uwezo wa adabu ya namna ya kutumia hiyo fedha katika malengo yaliyotarajiwa ili waweze kurejesha ili na wengine pia waweze kuchangamkia hizo fedha wakope pia” alisema Salali.

Aidha Mkurugenzi huyo wa Shirika lisilola kiserikali la FDH amewataka watu wenye ulemavu wasijinyanyapae wenyewe kwa namna yoyote pale walipo bali wachangamkie fursa mbalimbali za maendeleo kule walipo.

Alisema Kuna baadhi ya wenye ulemavu hujinyanyapaa wenyewe kwa ulemavu walionao katika jamii zao waache tabia hiyo bali jamii yote ya wenye ulemavu na wasio na ulemavu wana haki sawa katika jamii.

Hatahivyo ameomba pia jamii kuto kuwabagua watu wenye ulemavu na kutokuwafanyia vitendo vya ukatili.

Alisema shirika hilo la FDH kwakushirikia na Women Fund Tanzania Trust katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wamekuwa wakiwafundisha wenye ulemavu namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili, namna ya kuripoti polisi wakifanyiwa vitendo vya ukatili na hatua zipi wanapaswa kuchukua wakifanyiwa ukatili”

“Tunataka ushiriki wa watu wenye ulemavu katika mambo mbalimbali na nyanja tofauti tofauti kama masuala ya uongozi tuwaone watu wenye ulemavu,wanashiriki bila

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!